Video ya kasisi akimpaka mafuta mwanamke kwenye matiti na sehemu za siri yazua hisia mseto

Mchungaji huyo alisikika akimuombea mwanamke huyo huku akipitisha mikono yake kwenye miguu na sehemu zake za siri.

Muhtasari

•Katika video hiyo, mwanamke anaonekana akiwa amejilaza chali huku akimsimulia kasisi kuhusu tukio lake na mganga.

•Mwanamke huyo alimuonyesha kasisi sehemu za mwili ambazo mganga alipaka mafuta ili kumfanya avutie kwenye macho ya mume wa mwanamke mwingine.

Image: HISANI

Video ya mwanaume anayedaiwa kuwa mtumishi wa Mungu akimuombea mwanamke mmoja huku akimpaka mafuta sehemu mbalimbali za mwili wake imeendelea kuvuma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Mwanahabari wa Kikuyu Nyoxx Wa Katta alishiriki video hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook na kutoa tahadhari kwa mashabiki wake kuzingatia ni kina nani wanaamini na masuala yao ya kiroho

Katika video hiyo, mwanamke anaonekana akiwa amejilaza chali huku akimsimulia kasisi kuhusu tukio lake na mganga. Kasisi huyo anaonekana akimpaka mafuta mwilini huku wakiendelea kuzungumza.

“Nilienda kwa mganga, nikapakwa, nikapendeza, nikapendeza. Nikamchukua, nikamchukua, nimempata,” alisikika mwanamke huyo akimwambia kasisi.

Mwanamke huyo aliendelea kumwonyesha mchungaji sehemu za mwili ambazo mganga alipaka mafuta yasiyojulikana ili kumfanya avutie kwenye macho ya mume wa mwanamke mwingine.

Wakati mwanamke huyo akionyesha sehemu za mwili alizopakwa mafuta na mganga, mchungaji alionekana akinyunyiza mafuta na kutumia mikono yake kuyatandaza. Miongoni mwa sehemu za mwili alizoonyesha ni pamoja na tumbo, matiti na mapaja yake.

“Kabla uende, ati ulishika bwana ya wenyewe? Hutaki ndoa ya huyo mwanamke? Anaringa? Mwanamke anaringa? Sasa utaachilia huyo mwanaume wake?” mchungaji alisikika akimhoji mwanamke huyo.

Alipohojiwa zaidi, mwanamke huyo alidai kuwa alimlipa mganga huyo Ksh2000 kwa huduma hizo.

Alisema mganga huyo alimwambia maneno kadhaa na kumuahidi kuwa angemvutia sana mwanaume huyo ambaye alikuwa akimlenga.

“Aliniambia ni vizuri niwe nimependeza. Nikikaa nay eye kwa gari, atanipenda. Alinipenda hivyo bure,” mwanamke huyo alisema.

Mtumishi huyo wa Mungu aliendelea kumuombea mwanamke huyo kwa lugha ya Kikuyu huku akipitisha mikono yake kwenye miguu yake na sehemu zake za siri.

Video hiyo ambayo sasa imesambaa kwenye mitandao ya kijamii imezua hisia tofauti kutoka kwa watumiaji wa mtandao. Tazama maoni ya baadhi ya watumiaji wa Facebook;-

Njora wa Wanjiru: Sasa haya ni mambo gani? Watu kukosa heshima kwa Mungu.

Justina Wamae: I now see why husbands are saying wives should stop going to church because the risk of losing the wife to a spiritual person is higher than losing her out here 😂😂😂😂

Anna Blessed Wa Steve: This is immorality.

Mbote Njogu: Nataka kuwa pastor sasa.

Fabby Fabbiano KE: The lady and the pastor should be arrested.

Julii Blessed: He seems to be enjoying.