“Heshima imekosekana, I’m single! Zuchu atangaza mwisho wa mahusiano yake na Diamond

Zuchu alifichua kuwa uhusiano huo wao wa kimapenzi umefikia kikomo akidokeza kuwa Diamond amemkosea heshima.

Muhtasari

• Zuchu ametangaza rasmi kuvunjika kwa ghafla kwa uhusiano wake wa kimapenzi na bosi wake Diamond Platnumz.

•Tangazo hili limekuja saa chache baada ya Diamond kuonekana akiwa ameshikana mikono kimahaba na Zari Hassan.

katika ziara yao ya Ufaransa.
Diamond Platnumza na anayedaiwa kuwa mpenziwe, Zuchu katika ziara yao ya Ufaransa.
Image: INSTAGRAM// ZUCHU

Malkia wa Bongofleva, Zuhura Othman almaarufu Zuchu ametangaza rasmi kuvunjika kwa ghafla kwa uhusiano wake wa kimapenzi na bosi wake Diamond Platnumz.

Katika taarifa yake Ijumaa jioni, mwimbaji huyo mzaliwa wa Zanzibar alikiri kuwa kwa muda mrefu amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na bosi huyo wa WCB.

Hata hivyo, alifichua kuwa uhusiano huo uliozungumiwa sana kote barani Afrika umefikia kikomo akidokeza kuwa Diamond amemkosea heshima.

“HABARI FAMILIA .ILIBIDI KUPOST HII ILI KUFUTA DHAMIRI YANGU. KUANZIA LEO HII MIMI NA NASIBU (DIAMOND) HATUKO PAMOJA,” Zuchu alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Aliongeza, “NAJUA HILI LIMEKUWA JAMBO LETU LAKINI AS HARD AS IT IS KUMUACHA MTU UNAEMPENDA HII NAOMBA MUNGU IWE YA MWISHO NA NIANZE MAISHA MAPYA. MAPENZI NI HESHIMA KWA BAHATI MBAYA SANA HIKO KIMEKOSEKANA KWETU.”

Licha ya kusambaratika kwa uhusiano wao wa kimapenzi, Zuchu hata hivyo aliweka wazi kuwa wataendelea kufanya kazi pamoja katika WCB.

Binti huyo wa Khadija Kopa alitangaza kuwa sasa yuko single akibainisha wazi kuwa yuko tayari kwa sura mpya ya maisha yake kama mtu huru.

“NAMTAKIA YEYE NA FAMILIA YAKE KILA LA KHERI KABISA .TUMEISHI VIZURI LAKINI NADHANI HII SIO RIZKI .MWAKA HUU NIMEJIFUNZA KUSEMA HAPANA KWA KILA KITU KISICHONIPA FURAHA AMA BAADA YA KUSEMA HAYA NAONA KABNYE MASHAURI YA KUFURAHIA NA KUFURAHIA MPAKA . . KWA SASA KAZI IENDELEE NA MIMI NIKO SINGLE ���.,” Zuchu alisema.

Tangazo hili limekuja saa chache baada ya Diamond Platnumz kuonekana akiwa ameshikana mikono kimahaba na mzazi mwenzake Zari Hassan.

Siku ya Alhamisi jioni, video inayomuonyesha bosi wa WCB Diamond Platnumz akitembea huku akiwa ameshikana mikono na mzazi mwenzake Zari Hassan ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Staa huyo wa bongofleva alikuwa wa kwanza kuchapisha video hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alimtambulisha mama huyo wa watoto wake wawili kama dada yake.

“Mimi na dada @zarithebosslady,” Diamond aliandika chini ya video hiyo.

Video hiyo iliyosambazwa ilizua hisia mseto kutoka kwa wanamtandao tofauti ambao walitaka kuelewa kilichokuwa kikiendelea.

Zari alijibu, “aaai, nimekufa.”