(Video) Mume agundua mkewe amekua akitumia ARVs kisiri kwa miaka 3 kwenye ndoa

“…kwa hiyo mimi sasa ni kama chombo cha matumizi kwake, Haja hajali kuhusu watoto wetu ambao bado wananihitaji, ni wachanga bado. Nashukuru Mungu kwa huu ufunuo,” mwanamume huyo alisema

Muhtasari

• Alielekeza kamera kwenye kochi la sebuleni na kuonyesha jinsi mkewe alitoboa kochi na kutengeneza shimo ambalo anaficha vidonge hivyo.

Mwanamume mwenye huzuni na mfadhaiko.
Mwanamume mwenye huzuni na mfadhaiko.
Image: Maktaba

Mwanamume mmoja nchini Uganda amepigwa na butwaa baada ya kugundua kwamba mkewe amekuwa akitumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI, ARVs kwa muda mrefu wakiwa katika ndoa.

Mwanamume huyo alikuwa anachakura nyumbani kwake na kuvipata vidonge kadhaa vya ARV kwenye mkebe na akarekodi kwenye video akisema kwamba ni ufunuo ambao aliletewa na Mungu.

“Hii ni risti hapa, kuna kitu Fulani ambacho nataka kuwaonyesha ambacho mke wangu amekuwa akinificha kwa miaka yote 3 kwenye ndoa. Katika maombi yangu Mungu amenipa ufunuo, na leo ninakwenda kumuanika. Ninamshukuru Mungu kwamba nilipata ukweli huu,” mwanamume huyo alisema huku akiendelea kuchakura Zaidi kwenye vitu vya mkewe.

Alielekeza kamera kwenye kochi la sebuleni na kuonyesha jinsi mkewe alitoboa kochi na kutengeneza shimo ambalo anaficha vidonge hivyo vya ARV kwa muda wote bila yeye kujua.

Mume agundua mkewe amekuwa akitumia vidonge vya ARVs
Mume agundua mkewe amekuwa akitumia vidonge vya ARVs
Image: Screengrab

Baada ya kufunua shimo katika kochi hilo, alivuta mkebe ambao ulikuwa umejazwa vidonge vyeupe na kudai kwamba ni ARVs.

“Hizi ni ARVs, na hili ni onyo kwa wale ambao wanataka kuingia katika ndoa. Nilimuamini na moyo wangu wote, nilisafiri na yeye kwa magonjwa yote na matatizo yangu yote, lakini hiki ndicho amenifanyia kinyemela, anatumia ARVs huku mimi akinianika kwa maambukizi bila kujali kama nakufa ama naishi.”

“…kwa hiyo mimi sasa ni kama chombo cha matumizi kwake, ananitumia kimasihara. Haja hajali kuhusu watoto wetu ambao bado wananihitaji, ni wachanga bado. Nashukuru Mungu kwa huu ufunuo,” mwanamume huyo alisema kwa sauti iliyonyong’onyea huku akivirudisha vitu vya mkewe sehemu vilipokuwa.