Sandra Dacha ashangaa mbona wafu huvalishwa suti ndani ya jeneza

“Mimi nayo nashangaa mbona asivalishwe jezi ya mpira na wamalizane naye apumzike. For instance kama ni wa Manchester piga yeye Red,“ Wuod Ogomah alipendekeza.

Muhtasari

• “Suti ndio inakubaliwa pale ofisini mwa yesu soma bibilia wewe!!!!” Azlinh Jabocha alimjibu.

SANDRA DACHa
SANDRA DACHa
Image: FACEBOOK

Muigizaji Sandra Dacha amezua mjadala pevu katika ukurasa wake wa Facebook baada ya kuibua swali ambalo limekuwa likimtatiza akili kwa muda mrefu.

Dacha anashangaa na kukosa kupata jibu kuhusu ni kwa nini marehemu aghalabu huvalishwa suti wakiwa wamelzwa ndani ya jeneza.

Muigizaji huyo aliuliza swali hilo huku akipendekeza kwamba watu ambao wamekufa hutajwa kuwa ‘wamepumzika katika usingizi wa milele’ na hivyo wanafaa kuvalishwa pajama za kulala badala ya suti.

“Lakini sijawahi elewa mbona mtu avalishwe suti akiwa kwa jeneza/casket badala tu ya pajamas😶” Sandra Dacha aliuliza na kupendekeza kwa wakati mmoja.

Hata hivyo, maoni na majibu ya kuchekesha na kushangaza yalishuhudiwa kutoka kwa wafuasi wake, baadhi wakimuunga mkono na wengine wakitoa sababu ambazo wanahisi ndio sababu ya marehemu kuvishwa suti.

“Suti ndio inakubaliwa pale ofisini mwa yesu soma bibilia wewe!!!!” Azlinh Jabocha alimjibu.

“Unaimagine ukitokelezea mbinguni ama kwa shetani na Pajama?” kinyanjui Mbugu alisema.

“Mimi nayo nashangaa mbona asivalishwe jezi ya mpira na wamalizane naye apumzike. For instance kama ni wa Manchester piga yeye Red,“ Wuod Ogomah alipendekeza.

“Harusi ya mwisho yayeee...pajamas for wuot” Charlot Dulo.

Kwa upande wako unahisi kwa nini marehemu wengi huzikwa na suti?