Video ya mwanawe Bernice Saroni akibubujikwa machozi baada ya kuhojiwa kuhusu babake yaibua hisia

Alipoulizwa kwa nini analia, mvulana huyo alisema, “Kwa sababu simfahamu baba yangu tena."

Muhtasari

• Bi Saroni anayejitambulisha kama Mamake Boyz alisikika akimuuliza mwanawe jinsi anavyohisi kutokuwa na baba.

•Mada hiyo ilionekana kumgusa sana mtoto huyo hadi akaanza kutoa machozi bila kujizuia huku mama yake akiendelea kuzungumza.

Image: TIKTOK// MAMAKE BOYZ

Video ya kihisia ya mtoto wa Bernice Saroni akilia baada ya mtayarishaji huyo wa maudhui kumuuliza kuhusu baba yake imezua hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo iliyochapishwa kwenye akaunti yake ya tiktok, Bi Saroni anayejitambulisha kama Mamake Boyz alisikika akimuuliza mwanawe jinsi anavyohisi kutokuwa na baba.

Wawili hao walikuwa wamekaa ndani ya gari wakati binamu huyo wa Samidoh alisikika akimuonya mwanawe kuhusu unyeti wa majadiliano ambayo alitaka washiriki kabla ya kuuliza swali lake.

“Junior, nataka nikuulize swali leo. Kaa nyuma, ni kitu nyeti sana. Unajisikiaje kama huna baba?" Bi Saroni alisikika akimuuliza mwanawe.

Mvulana huyo mdogo ambaye alikuwa amekaa kiti cha nyuma cha gari alionekana kufikiria sana juu ya swali hilo kabla ya kusema kwamba hajui anachohisi.

Mama huyo wa wavulana wanne anayeishi Marekani hata hivyo alisisitiza kujua hisia za mwanawe kuhusu kutokuwa pamoja na mzazi wake mwingine.

“Unapowaona watoto wengine wakiwa na baba yao, unajisikiaje?” Aliuliza tena.

Ilikuwa wakati huo ambapo 

Mada hiyo ilionekana kumgusa sana mtoto huyo kiasi kwamba alianza kutoa machozi bila kujizuia huku mama yake akiendelea kuzungumza.

"Ukimuona baba yako leo, utamjua?" Bernice aliuliza.

Mvulana huyo alikiri kwamba hataweza kumtambua baba yake ikiwa angemwona leo, kwani ni muda mrefu tangu amwone uso kwa uso.

Alipoulizwa kwa nini analia, mvulana huyo alisema, “Kwa sababu simfahamu baba yangu tena."

Bi Saroni alijaribu kumfariji kwa kumwambia kwamba yupo kwa ajili yake na kwamba anampenda sana.

“Unajua nakupenda sana, unamuona (baba yake) kwenye picha. Nimekuonyesha baba yako kwenye picha, sawa?" alimwambia mwanae.

Junior akamjibu, "Ndiyo, lakini anaweza kuonekana tofauti."

Bi Saroni hata hivyo alimfahamisha kuwa huenda sura ya babake haijabadilika sana.

“Usijisikie vibaya. Nakupenda sana,” alisema.

Video hiyo imeendelea kuibua hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya wanamtandao wakimkosoa mama huyo wa watoto wanne, wengine wakimtetea na wengine hata kumuonea huruma mtoto huyo.