“Osha vyombo, fua, pika…” Mrembo ashauri watu wasio na kazi ambao ‘wanawekwa’ (video)

“Sio unaishi na mtu halafu siku nzima unakaa sebuleni na rimoti mkononi ukisema jinsi ulivyo na stress, halafu nikipika unataka kula, mimi nimetoka nimeleta chakula halafu tena nikupikie, rafiki yangu, hapa sio hotelini,” aliongeza.

Muhtasari

• "Halafu baada ya mwezi mmoja au miwili unaenda unaanza kusema eti nilikuwa nakusema, eti hukuwa na uhuru," alisema.

Mrembo ashauri watu wanaowekwa
Mrembo ashauri watu wanaowekwa
Image: TIKTOK

Mrembo mmoja mwenye umri wa makamo katika mtandao wa video fupi wa TikTok kwa jina Zoe Favour Backup amezua utata katika mtandao huo baada ya kupakia video akitoa ushauri kwa watu wanaishi maisha mazuri kwa ‘kuteleza kwa ganda la ndizi’.

Mrembo huyo aliwashauri watu hao ambao hawapendi kufanya kazi na wanategemea wenyeji wao kuwahudumia nyumbani kujituma katika kufanya kazi za ndani kama njia moja ya kumpa motisha e anayemfuga kama njiwa.

Alisema kwamba mgeni kama unaishi kwa kutegemea mwenyeji wako, tena amekuweka kwake, kila siku akiondoka kwenda kazini basi ni jukumu lako kufanya kazi zote za ndani ikiwemo kufua, kupika, kuosha vyombo, kudeki nyumba na zingine.

“Sisemi hili kwa njia mbaya lakini kama unaishi na mtu na huna uwezo wa kumsadia katika majukumu ya kuendesha nyumba, basi jitume katika kufanya kazi za ndani. Osha vyombo, fua, pika… onyesha mwenyewe pia wewe unawajibika,” mrembo huyo alishauri.

“Sio unaishi na mtu halafu siku nzima unakaa sebuleni na rimoti mkononi ukisema jinsi ulivyo na stress, halafu nikipika unataka kula, mimi nimetoka nimeleta chakula halafu tena nikupikie, rafiki yangu, hapa sio hotelini,” aliongeza.

Alisema kwamba hiyo ndio njia pekee ya kumfanya mwenye nyumba kuwa na motisha wa kuendelea kuishi na wewe bila kuchoka, lakini ukitebwereka wewe ndio unakwenda huko nje kuanza kunadi kwamba ulikuwa unateswa kwa wenyewe.

"Halafu baada ya mwezi mmoja au miwili unaenda unaanza kusema eti nilikuwa nakusema, eti hukuwa na uhuru," alisema.

Tazama video hii hapa na utoe maoni yake kuhusu ushauri huu;