Amira afunguka jinsi talaka na Jimal iliwaathiri watoto wao hadi akalazimika kuwapeleka 'therapy'

Alisema baada ya ndoa kuvunjika, alipata amani, akapona na akawepo zaidi katika maisha ya watoto wake.

Muhtasari

•Alisema talaka ilikuwa na athari za kisaikolojia, sio kwake tu bali pia kwa watoto wake ambao ilibidi awapeleke kwa mtaalamu wa ushauri nasaha.

•Alidokeza kuhusu kumsamehe kila mtu aliyemkosea wakati ndoa yake ilipoharibika miaka michache nyuma.

Jimal Rohosafi na aliyekuwa mke wake Amira
Image: HISANI

Mfanyibiashara Amira amekiri kuwa talaka yake na mzazi mwenzake Jimal Rohosafi iliathiri watoto wao kisaikolojia.

Mama huyo wa watoto wawili alifichua hayo Jumatatu jioni baada ya kukutana na mume huyo wake wa zamani kuhusu masuala ya uzazi.

Alisema talaka yao ilikuwa na athari za kisaikolojia, sio kwake tu bali pia kwa watoto wake ambao ilibidi awapeleke kwa mtaalamu wa ushauri nasaha.

"Acha niwaaambie jinsi talaka ilivyoathiri watoto wangu hadi ikabidi niwapeleke kwa matibabu (Hata hivyo, hadithi ndefu kwa siku nyingine). Imenichukua kazi nyingi kuwa mahali nilipo kiakili." ” Amira alisema kupitia Instagram.

Mfanyibiashara huyo wa bidhaa za urembo aliendelea kudokeza kuhusu kumsamehe kila mtu aliyemkosea wakati ndoa yake ilipoharibika miaka michache nyuma.

"Kushikilia hasira na kinyongo hakunifanyii lolote jema. Mimi ni mtu huru, nilimwacha Mungu apigane vita vyangu na kulipiza kisasi kwa ajili yangu,” alisema.

Alisema baada ya ndoa yake kuvunjika, alipata amani, akapona na akawepo zaidi katika maisha ya watoto wake.

Wakati huo huo, aliwaonya wanamtandao dhidi ya kumfundisha jinsi ya kuwa mzazi mwenzake na mume wake wa zamani akisema yuko tayari kufanya lolote.

"Nitafanya chochote ninachoona kinafaa kwa ajili yangu, mradi tu iwe na heshima na amani kwa ajili yake. Nikiwa nimesema hayo, usiku mwema wapendwa. Wacha nimeze madawa nikalale,” Amira alisema Jumapili jioni.

Aliongeza, "Watu wale wale wanakuja kwenye Dm yangu kunifundisha jinsi ya kuwa mzazi mwenza ni wale wale ambao bado wangenipiga kama leo wangesikia kwamba Amira ni mama mtoto mbaya au X  mwenye machungu.

Guess what, naweza pia kunifanya. na nyote mtarekebisha, na ikiwa hamtafanya hivyo, ni sawa pia. Usijali, nimelia vya kutosha sitarudi kulia! Je, nilikuambia kuhusu Amira 2.0? ama nitajitambulisha tena?”

Amira alitoa matamshi hayo baada ya hisia mseto kuibuka kwenye mitandao ya kijamii kufuatia mkutano wake wa hivi majuzi na aliyekuwa mume wake Jimal Rohosafi.