Cebbie Koks ajibu baada ya dada yake Akothee kukejeliwa na bintiye, Rue Baby

Cebbie Koks alizungumza kuhusu picha fulani ya zamani ya dada yake ambayo ilifufua kumbukumbu za zamani.

Muhtasari

•Akothee na Cebbie Koks walitoa maoni baada ya binti mzaliwa wa mwimbaji huyo, Rue Baby kuchapisha video ya kumdhihaki.

•Mwanamuziki huyo ambaye alionekana kuelewa utani ndani ya video hiyo na alionekana kustaajabishwa tu.

katika picha ya maktaba.
Cebbie Koks na dadake mkubwa Akothee katika picha ya maktaba.
Image: INSTAGRAM//

Akothee na dada yake Elseba Awuor Kokeyo almaarufu Cebbie Koks walitoa maoni baada ya binti mzaliwa wa pili wa mwimbaji huyo, Rue Baby kuchapisha video ya kumdhihaki.

Siku ya Jumapili, Rue Baby alitumia ukurasa wake wa Instagram kushiriki video ya kusisimua inayoonyesha maendeleo ya mama yake tangu alipokuwa hajiwezi sana kifedha hadi sasa ambapo yeye ni miongoni mwa wasanii matajiri zaidi nchini Kenya.

“Samahani ooo,@akotheekenya Establisshh,” Rue Baby aliandika chini ya video aliyochapisha.

Video hiyo ilionyesha mkusanyo wa picha za Akothee kuanzia zile zilizopigwa wakati hakuwa katika hali nzuri ya kifedha na kumalizia na picha zake za sasa zinazomuonyesha akiwa katika hali nzuri.

Sauti ya kuchekesha inayozungumza kuhusu Esther kuwa mweusi na aliyefilisika katika siku za nyuma na baadayye kuwa sawa baada ya kupata pesa ilicheza kwenye video hiyo ya mkusanyiko wa picha.

“Esther was black and broke. But when Esther see money, Establisshhh,” sauti ya nyuma ilisema.

Kumaanisha: “Esther alikuwa mweusi na aliyefilisika. Lakini Esther alipoona pesa, Establisshhh"

Mwimbaji Akothee ambaye alikuwa akidhihakiwa kwenye video hiyo, na dada yake mdogo Cebbie Koks walikuwa miongoni mwa watu waliotoa maoni.

Mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni Esther Akoth Kokeyo alionekana kuelewa utani ndani ya video hiyo na alionekana kustaajabishwa tu.

"Lakini kwa nini ..." alisema.

Kwa upande wake, Cebbie Koks alizungumza kuhusu picha fulani ya zamani ya dada yake iliyoonyeshwa kwenye video ambayo ilimkumbusha kumbukumbu za zamani.

"Picha ya pili imenikumbusha mambo mengi… Awuoro jumper ya blue," Cebbie Koks alitoa maoni na kuambatanisha ujumbe wake na emoji za kucheka.

Tazama maoni ya baadhi ya wanamitandao wengine;-

julie_sakong: This is the real Esther that was being talked about.

cheptum_lashei: It be your own children! So says the legend.

turugamarie: Enyewe pesa ni mzuri, inaosha mwosho moja

karenzo.nyamu: Challenge closed

letoya_johnstone: One thing about Esther is that she is beautiful.