Sarah afichua maelezo kuhusu uhusiano wake na Diamond, azungumzia uwezekano wa kurudiana

“Hajawahi kusema anampenda mwingine zaidi yangu. Siku zote anasema nampenda Sarah kuliko mwanamke yeyote,” alijigamba.

Muhtasari

•Mrembo huyo alithibitisha kuwa yeye na bosi huyo wa WCB walichumbiana kwa takriban miaka mitatu.

•Alidai kuwa nyimbo zote kwenye albamu ya kwanza ya staa huyo wa bongo fleva ziliimbwa kwa ajili yake.

amefunguka kuhusu mahusiano yake ya zamani na Diamond Platnumz
Sarah amefunguka kuhusu mahusiano yake ya zamani na Diamond Platnumz
Image: HISANI

Sarah, mwanamke aliyemchochea staa wa bongofleva Diamond Platnumz kutunga wimbo ‘Kamwambie’ amefunguka kuhusu uhusiano wao wa siku za nyuma.

Akizungumza na waandishi wa habari za mitandaoni baada ya shoo ya Diamond ambayo alihudhuria mwishoni mwa wiki jana, mrembo huyo alithibitisha kuwa yeye na bosi huyo wa WCB walichumbiana kwa takriban miaka mitatu.

“Tumeishi kabisa. Kama miaka mitatu hivi. Toka 2006, 2007 hivi hadi 2009,” Sarah alisema.

Alibainisha kuwa Diamond Platnumz amekuwa akidai kumpenda kuliko mwanamke yeyote ambaye amekuwa naye kwenye mahusiano.

“Hajawahi kusema anampenda mtu mwingine zaidi yangu. Siku zote anasema nampenda Sarah kuliko mwanamke yeyote,” alisema.

Mwanadada huyo alidai kuwa mwanzoni Diamond alikuwa ameweka jina lake kwenye wimbo wa ‘Kamwambie’ kabla ya kuliondoa.

Pia alidai kuwa nyimbo zote kwenye albamu ya kwanza ya staa huyo wa bongo fleva ziliimbwa kwa ajili yake.

“Albamu yake ya kwanza, nyimbo zote nafikiri aliandika kwa ajili yangu,” alisema.

Sarah hata hivyo alibainisha kuwa yeye na mwimbaji huyo wa WCB hawana tena uhusiano wa kimapenzi, lakini badala yake, ni marafiki wakubwa.

“Kuachana sio vita, sisi ni marafiki. Nimetafutwa muda mrefu nifanye interview, sijui nini, mpaka mwenyewe alikuwa ananiambia naitwa na watu. Lakini sijawahi, nina aibu sana,” alisema Sarah.

Alifichua kuwa muda mrefu ulikuwa umepita tangu alipomwona Diamond mara ya mwisho.

“Mara nyingi Naseeb anaweza kukaa kimya muda mrefu na akanipigia. Anaweza akatafuta namba yangu akanipigia akaniambia ‘Sarah nimekukumbuka sana, njoo ata tuongee tusalimiane,” alisema.

Mfanyabiashara huyo wa nguo aliweka wazi kuwa hana nia ya kuchumbiana tena na Diamond.

“Naseeb ni mtu mzuri, ni rafiki yangu,” alisema.

Sarah pia aliweka wazi kwamba hahitaji chochote kutoka kwa Diamond akisema anajivunia mafanikio yake.