Wasiwasi huku gari la Diana Marua likipasuka tairi kwenye Thika Road, akwama na watoto

Diana alisema wakati alipogundua tairi lake lilikuwa limepasuka, tayari ilikuwa kuchelewa na gari halikuweza kusonga tena.

Muhtasari

•Bahati alilazimika kukimbia kumsaidia mkewe baada ya gari lake kupata tatizo na kukwama kwenye Barabara ya Thika siku ya Jumapili usiku.

•Bahati alisikika akielezea kisa hicho na pia kumshauri mke wake kile ambacho alipaswa kufanya baada ya tukio kutokea.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Mwimbaji wa Kenya Kelvin Kioko almaarufu Bahati alilazimika kukimbia kumsaidia mkewe Diana Marua baada ya gari lake kupata tatizo na kukwama kwenye Barabara ya Thika siku ya Jumapili usiku.

Bahati alichapisha video ya tukio hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram akionyesha jinsi gurudumu la mbele la gari la Diana aina ya Range Rover Vogue ya bluu lilivyopasuka na kumfanya asimame kwenye barabara.

Alimshukuru Mungu kwa kumlinda mke wake na watoto wao waliokuwa naye wakati wa tukio hilo huku akibainisha kuwa wote walikuwa wameingiwa na hofu.

"Mke wangu na watoto bado wako chini ya shambulio la hofu.. Hiki ndicho kilichowapata kwenye barbara ya Thika Super Highway.. Mungu ni mkubwa," Bahati alisema chini ya video aliyochapisha.

Katika video hiyo, mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili alisikika akielezea kisa hicho na pia kumshauri mke wake kile ambacho alipaswa kufanya baada ya tukio kutokea.

“Niko hapa kwenye Barabara ya Thika, Mvua inanyesha. Niko hapa kumwokoa Diana. Diana amekwama na watoto kwa Thika Super Highway,” Bahati alieleza.

Huku akimgeukia mkewe Diana, mwimbaji huyo alimwambia, “Sasa, kitu utafanya, utatoa watoto. Lakini babe, mtu akibondwa huenda pande ile nyingine. Mahali mko ni hatari, yaani ni Mungu amewasaidia. Ona watu wameegesha nyuma yenu. Mimi nilidhani ni nyinyi mmepata ajali.”

Diana alieleza kuwa kufikia wakati alipogundua tairi lake lilikuwa limepasuka, tayari ilikuwa kuchelewa na gari halikuweza kusonga tena.

Mamia ya mashabiki wamejitokeza kumfariji mama huyo wa watoto watatu baada ya tukio hilo la kutisha na pia kumshukuru Mungu kwa kuwaokoa.

Mnamo Oktoba mwaka jana, Bahati alimshangaza mkewe Diana Marua na gari mpya kabisa ya Ranger Rover Vouge Autobiography iliyohusika katika tukio hilo.

Diana alipoona gari hilo la Sh19, 000, 000, alilia kwa machozi ya furaha akikiri kwamba alikuwa haamini kwamba gari hilo ni lake rasmi.

"Hii ni Ranger Rover Vogue Autobiography mpya. Huu ndio mtindo bora na hizi ni funguo za gari lako. Ina vipimo maalum kwa ajili yako, mambo ya ndani ni mvinyo mwekundu uliogeuzwa kukufaa na kila kitu ni cha kipekee na gari hili ni moja tu nchini Kenya, lako pekee.,” Bahati alimwambia  mke wake Diana.

"Nilifanya nini ili kustahili haya yote…Siwezi hata kuamini…asante, Mungu," Diana Marua akilia alisikika akisema.

Hii ilikuwa ni zawadi namba saba, ambayo Bahati alikuwa amempa mkewe walipokuwa wakisherehekea miaka saba ya ndoa.