Manzi wa Kibera afunguka jinsi alivyokutana na marehemu Mzee Nzuki

Mwanasosholaiti Manzi wa Kibera amefunguka kuhusu uhusiano wake halisi na marehemu Mzee Nzuki.

Muhtasari

•Aliweka wazi hakuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Nzuki, akibainisha walikuwa wakiigiza tu vipindi kwa ajili ya burudani ya mtandaoni.

•Alifichua kuwa Mzee Nzuki alikubali kucheza naye vipindi na walikuwa na muungano mzuri punde walipoanza.

Manzi wa Kibera na Mzee Sammy Nzuki
Manzi wa Kibera na Mzee Sammy Nzuki
Image: INSTAGRAM

Mwanasosholaiti mashuhuri wa Kenya Sharon Wambui almaarufu Manzi wa Kibera amefunguka kuhusu uhusiano wake halisi na marehemu Mzee Sammy Ndunda Nzuki.

Katika mahojiano ya hivi punde na Oga Obinna, mrembo huyo kutoka mtaa wa Kibera aliweka wazi kuwa hakuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Nzuki, akibainisha kwamba walikuwa wakiigiza tu vipindi kwa ajili ya burudani ya mtandaoni.

Alifichua kuwa alihisi hamu ya kuzua drama kwenye mitandao ya kijamii na hivyo akaamua kutafuta mwanamume mzee sana wa kuigiza kama mpenzi wake.

“Vipindi zote nilikuwa nimewaonyesha katika tasnia hii, mimi ndo nilikuwa kusema. Yaani nilikuwa nimechafua hewa kisha nikasema, nahitaji sana kuchafua hewa zaidi kwa watu hawa. Nilienda ghetto nikaona nahitaji mwanaume mzee sana.

Nilitaka mwanaume mzee kuliko huyo maze lakini hakupatikana, huyo (Nzuki) ndiye mwanaume aliyepatikana,” Manzi wa Kibera alisema.

Aliongeza, “Nilitaka mwanaume mzee sana, yaani namshika nambeba kwa mgongo. Nilituma mtu aende anitafutie wanaume wawili wazee kisha nichague mmoja. Nikaletewa wawili, mmoja alikuwa Mluo na alikuwa anaongea sana. Nilisema huyu siwezi piga naye kipindi atachoma, ataambia Waziri wa Habari kila kitu.”

Mwanasosholaiti huyo aliyezingirwa na utata mwingi alifichua kuwa Mzee Nzuki alikubali kucheza naye vipindi na walikuwa na muungano mzuri punde walipoanza.

Wiki jana, iliripotiwa kwamba Manzi wa Kibera hakuhudhuria maziko ya marehemu Mzee Nzuki yaliyofanyika Jumatano, Mei 1.

 Katika video iliyovuja mtandaoni, ni watu wachache tu waliohudhuria hafla ya maziko ya mzee huyo mwenye umri wa miaka 67 kwenye makaburi ya Langata.

Sammy Ndunda Nzuki alifanyiwa hafla rahisi ya maziko.

Chali wa Kibera aliibuka na kufichua kuwa Manzi wa Kibera almaarufu Wambo hakuwa sehemu ya maziko hayo. Yeye ni meneja wake.

"Nataka tu kuwajulisha kuwa Mzee Nzuki alizikwa leo Langata na hakukuwa na vyombo vya habari kwa sababu familia haikutaka uwepo wa media, walikua tu kutaka kumpatia mzee mazishi yenye heshima isiyo na kamera," Chali wa Kibera alieleza.

Aliongeza, “Ingawa nina video na picha chache lakini naomba niwafahamishe kuwa mzee amezikwa leo huko Langata na familia yake na mimi au Manzi wa Kibera hakuna aliyealikwa na ninaelewa kabisa maana labda walidhani tukienda tunaeza enda na. watu wa media."

Chali wa Kibera alishiriki maelezo ya hatua yao inayofuata akisema, "Labda tutapata muda wetu wa kwenda kuangalia kaburi ambayo walisema ni sawa,"