Ex wa Baha Georgina Njenga adokeza mahusiano mapya, akiri amepagawa na mpenziwe

Haya yanajiri takriban mwaka mmoja baada ya kuthibitisha kutengana na muigizaji Tyler Mbaya almaarufu Baha.

Muhtasari

•Mama huyo wa binti mmoja alichapisha picha yake nzuri akiwa ameketi kwenye meza iliyozungukwa na mazingira mazuri.

•Georgina hata hivyo hakushiriki maelezo zaidi kuhusu uhusiano huo mpya aliodokeza au mwanamume aliyezungumziwa

Image: INSTAGRAM// GEORGINA NJENGA

Mtayarishaji wa maudhui maarufu wa Kenya Georgina Njenga amedokeza kuhusu uhusiano mpya.

Siku ya Jumatano, mama huyo wa binti mmoja alichapisha picha yake nzuri akiwa ameketi kwenye meza iliyozungukwa na mazingira mazuri.

Chini ya picha hiyo, aliambatanisha na picha nyingine iliyokuwa na maandishi yanayozungumza kuhusu kushikwa na mwanaume mpya.

"Kwa kweli ninapagawa na mwanaume wangu," maandishi kwenye picha iliyoshirikiwa na Georgina Njenga yalisomeka.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 22 hata hivyo hakushiriki maelezo zaidi kuhusu uhusiano huo mpya aliodokeza au mwanamume aliyezungumziwa.

Haya yanajiri takriban mwaka mmoja baada ya mama huyo wa binti mmoja kuthibitisha kutengana na muigizaji wa zamani wa Machachari Tyler Mbaya almaarufu Baha.

Mapema mwaka huu, mtayarishaji huyo wa maudhui aliweka wazi kuwa yeye bado hana mpenzi lakini hatafuti. Alifichua hayo wakati wa mahojiano na mwanahabari Nicholas Kioko baada ya kuhojiwa kuhusu hali ya uhusiano wa  ex wakeTyler Mbaya.

Mama huyo wa binti mmoja alibainisha kuwa hawezi kujua ikiwa mzazi mwenzake, Tyler Mbaya amesonga mbele na maisha yake au la, lakini pia akathibitisha kuwa yeye yuko peke yake lakini hatafuti mpenzi.

"Sijui kama amemove on lakini mimi niko soko...bado sijapata mpenzi lakini sitafuti... Niko soko kujitafuta, na kugrow," alisema.

Georgina pia alifafanua kuwa chapisho lake la hivi majuzi kuhusu kuchumbiana na mwanamume asiye tajiri lilitafsiriwa vibaya na watu lakini akaeleza kuwa hatajali kukua na mwanaume.

"Kwa kweli lilikuwa swali. Naamini katika kufanya kazi kwa bidii, na ninaamini kabisa kukua na mtu. Siamini kwamba kulipa bili ni jukumu la jinsia. Ama kama msichana nafaa kuwa na mtu mwenye ananitumia kiasi fulani. kwa mwezi. Ikibidi uifanye kwa sababu ya kufanya, ifanye kwa sababu unanipenda," Alisema.

Alisema zaidi kwamba alitamani maisha yake na baba ya mtoto wake.

"Ndio kweli lakini maisha yalitokea, mambo yalitokea hivyo tunaendelea. Kitu kimoja cha maisha ni maisha yanasonga mbele, maisha yanaendelea hivyo hata nikimmiss, hizo ni kumbukumbu na angalau Astara atakua anasema tulikuwepo."

Georgina pia alifichua kwamba mipango ya baadaye ya uhusiano wake na Tyler haijulikani lakini akabainisha kuwa sura hiyo haikufungwa kabisa.

"Nadhani ningesema hujui na maisha. Huwezi pangia life. Leo naeza kuwa nimeplan hatutarudiana alafu turudiane ama niseme hapa hatuezi rudiana nayeye alafu turudiane. Ama niseme tunaeza rudiana alafu tukose. But of cause, destiny holds its place so maybe its place so maybe rudiana nayeye alafu turudiane. siku moja.

Kama vile sina mpango kuhusu maisha yangu. Nita panga ndio lakini Mungu ndio ako na ufunguo mkuu kwa hivyo labda ndio, labda hapana, lakini ni kitu ambacho sijafunga kabisa kutoka kwa sura yangu," Georgina alisema.