Wanawake wanaopenda mapishi huwavutia zaidi wanaume kwa ndoa kuliko wanawake wasomi

Alisema wanaume wengi ni heri waishi na mwanamke ambaye hana taaluma yoyote lakini anapenda kuwajibika jikoni kuliko kuishi na mwanamke msomi ambaye muda wote ananunua chakula mtandaoni ama kutegemea kijakazi kupika.

Muhtasari

• Hata hivyo, baadhi ya watu walipingana naye wakisema kuwa hulka ya wanaume hata ukimfanyia vizuri aje bado lazima atachepuka.

Image: GETTY IMAGES

Mwanaume mmoja amezua tafrani katika mtandao wa Facebook baada ya kuibuka na kile alichokiita utafiti wake kuhusu chaguo la asilimia kubwa ya wanaume katika suala zima la ndoa.

Mwanamume huyo kwa jina Nelson alisema kwamba idadi kubwa ya wanaume ambao wamefikia uamuzi wa kutafuta mwenzi na kutulia kwenye ndoa bila kushrutishwa huangazia Zaidi upande wa warembo wanaopenda mapishi ikilinganishwa na idadi ya wanaume wanaochagua wanaume wasomi.

Jamaa huyo alisema kwamba wanaume wengi ni heri waishi na mwanamke ambaye hana taaluma yoyote lakini anapenda kuwajibika jikoni kuliko kuishi na mwanamke msomi ambaye muda wote ananunua chakula mtandaoni ama kutegemea kijakazi kupika.

Nelson Igboke anahisi kwamba mwanamume mwenye mwanamke asiye na taaluma yoyote lakini anapenda mapishi ni moja kati ya wanaume wenye bahati adimu sana kupatikana, kwani hao ndio wanaojua furaha halisi ya ndoa.

Anaamini kwamba mwanamke kama huyo ni wa thamani zaidi kuliko mwanamke anayezingatia kazi yake.

“Mmoja wa wanaume waliobahatika zaidi duniani ni yule anayeoa mwanamke ambaye hobby yake ni kupika! Yeye ni wa thamani zaidi kuliko mwanamke mwenye taaluma. Niulize nikuambie,” aliandika.

Hata hivyo, baadhi ya watu walipingana naye wakisema kuwa hulka ya wanaume hata ukimfanyia vizuri aje bado lazima atachepuka.

Tazama chapisho hili hapa chini utoe maoni yako