Mchungaji Kanyari ataka msamaha kutoka kwa Prince Mwiti

"Nitakutumia 200k ukiniomba msamaha kwa mpesa ama niongeze ifike 400k"

Muhtasari

•Mwiti  alisema kuwa Kanyari ni mlaghai na akamuonya mhubiri huyo  asithubutu kumuibia nyota yake mwiti.

•Price Mwiti na Mchungaji Kanyari walizozana kwenye TikTok moja kwa moja baada ya Mwiti kushutumu maisha ya mchungaji huyo.

MCHUNGAJI VICTOR KANYARI
MCHUNGAJI VICTOR KANYARI
Image: MAKTABA

Mhubiri mwenye utata Mchungaji Victor Kanyari alitaka msamaha kutoka kwa Prince Mwiti baada ya kumtusi kwenye mtandao wa TikTiok.

Mwiti alichukua  mtandao wake waTikTok kumvua nguo mhubiri huyo kwa maneno yake akimtaja Kanyari kuwa mwizi.

“Uliibia watu pesa, ukaibia watu nyota halafu ukaja kujifanya nabii wa uongo, wewe ni mmoja wa manabii wa uongo hapa, tayari Bwana amejiweka mbali nawe, unanilaani, unamhutubia nani hapa TikTok. ?

Natumai kuwa  kile unaanza unaweza kukimaliza. Je, ni kwa sababu ilikuwa vigumu kwako kuiba nyota yangu? ."

Kanyari alizungumzia suala hilo kupitia mtandao wake wa TikTok, akisema kwamba alikasirishwa na TikToker huyo.

“Leo nahutubia Mwiti, leo nilikuwa nimekasirika sana, Mungu akanijia, nikakuona umepiga magoti mbele yangu, Nikaona ukiniomba ukisema nabii usinitumie kinyunyu, nilikuwa nikutumie kitu ukiwa umelala na lini unaamka ungeuliza umepatwa na nini, Mungu aliniambia nisitoe panga nililotaka kuua lakini Mungu aliniomba nikusamehe.