logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pasta asitisha utoaji sadaka katika kanisa lake, akiri waumini wanapitia maisha magumu kiuchumi

"Njoo ukamtumikie Mungu wako na uende; mpaka petroli ishuke; Si rahisi.” alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 May 2024 - 10:28

Muhtasari


  • • Alidai kuwa gharama ya usafiri tayari ni kubwa mno kwa waumini husika kumudu kwa urahisi na bado wanaweza kuchangia kifedha kanisani.

Mchungaji mmoja amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya video kuenezwa kutoka kwa mahubiri yake akitangaza kusitishwa kwa shughuli za utoaji sadaka katika kanisa lake.

Kwa mujibu wa mchungaji huyo ambaye hajabainika kwa jina, katikati mwa mahubiri yake, alitangaza kwamba shughuli za utoaji sadaka zilikuwa zimesimamishwa katika kanisa lake kwa kipindi cha sasa, akisema kwamba anaelewa fika jinsi waumini wengi wanapitia wakati mgumu kiuchumi kupata pesa.

 Mchungaji huyo aliwarai wachungaji wenzake kutoka makanisa mbalimbali pia kufuata mkondo huo na kuwaondolea waumini mzigo wa kutoa sadaka kwani hali ya uchumi wa nchi ni ngumu na wengi wanapitia nyakati ngumu kupata hata pesa za kununua vyakula nyumbani mwao.

Alidai kuwa gharama ya usafiri tayari ni kubwa mno kwa waumini husika kumudu kwa urahisi na bado wanaweza kuchangia kifedha kanisani.

Kwa maneno yake;

"Hatupaswi kukusanya matoleo leo. Kwa sasa, kwa sababu ya hali ya nchi hii, tunasubiri kutoa. Wachungaji wote wanapaswa kutambua, wakisubiri hali ya nchi hii kuimarika, hawapaswi kukusanya sadaka.”

"Fikiria mtu akija kanisani, akipanda teksi na 1,500 na bado anaacha sadaka, anaweza kuishia kurejea nyumbani. Je, hiyo ni akili? Ikiwa hutaacha pesa, haimaanishi kuwa mchungaji hatakula. Njoo ukamtumikie Mungu wako na uende; mpaka petroli ishuke; Si rahisi.”

Alimalizia kwa kuyataka makanisa mengine kufuata vivyo hivyo, “Kwa wachungaji wote, acheni kukusanya sadaka kwa sasa.”

Tazama video hapa chini…


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved