Mchungaji Kanyari akabidhiwa kondomu, arimis kama zawadi wakati wa ibada kanisani

Faith kisha alikiri kuwa aliota kuwa yeye na Kanyari walikuwa na harusi kubwa.

Muhtasari

•TikToker Faith Peters alimzawadia mhubiri huyo mwenye utata zawadi tatu, miongoni mwao ikiwa ni pakiti ya mipira ya kondomu, kabla ya kukiri kumpenda.

•Vitendo vya Faith vilizua hisia tofauti kwa wanamtandao, huku baadhi wakimlaumu kwa kutoliheshimu Kanisa.

MCHUNGAJI VICTOR KANYARI
MCHUNGAJI VICTOR KANYARI
Image: MAKTABA

TikToker wa kike aliyetambulika kwa jina la Faith M Peters aliwaacha wengi kwa mshangao baada ya kufika kanisani kwa Mchungaji Kanyari na kumzawadi mhubiri huyo zawadi tatu moja wapo ikiwa pakiti ya kondomu.

Mfanyabiashara huyo alimpa Kanyari kifurushi kidogo kilichokuwa kimefungwa kwenye gazeti. Alipofungua, Kanyari, ambaye alikuwa amesimama kwenye madhabahu, alionyesha  vitu hivyo tatu: kotex  liner, arimis petroleum jelly na pakiti ya kondomu.

Faith kisha alikiri kuwa aliota kuwa yeye na Kanyari walikuwa na harusi kubwa. Mwanamke huyo jasiri alibaini kuwa alifahamu kuwa wanawake wengi walikuwa wakipenda mapenzi ya Kanyari, na akamshauri kutumia kinga.

"Naona wanawake wanataka sana Pastor Kanyari, nimkuletea kinga ya maisha. Tumia kinga baba, usikatae wanawake," alisema.

 Faith alidai kumpenda mhubiri huyo mwenye utata, akimsihi amuoe.

 “Nataka utoke pale kwa Rish Kamunge kuja hapa. Watoto zaidi kwa hawa watoto wa Marekani tutaongeza nimechoka," alisema.

Vitendo vya Faith vilizua hisia tofauti kwa wanamtandao, huku baadhi wakimlaumu kwa kutoliheshimu Kanisa.

Monique's Danielson :

     "Eiish mnaeenda spidi sana. Hamuogopi hata man of God.

Mercy Mutuli :

   "Ooh God, have mercy upon us."

 Ngetich Langat Jeff :

    "That was the best gift ever been awarded ."

Festus Murithi Poul :

   "Condom kwa kanisa ?? Pastor yawa."

 Pappa Samwely Comedian :

   "The lady may be signifying something about."

Shiku Philip :

      "This is too much."