Guardian Angel ataja matakwa 3 maalum kwa ndoa yake huku mkewe Esther Musila akitimiza miaka 54

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ameelezea safari yake na Bi Musila kuwa ya ajabu.

Muhtasari

•Guardian Angel amezungumzia athari nzuri ambazo mkewe ameleta katika maisha yake katika miaka minne iliyopita ambayo wamekuwa pamoja.

"Cheers kwa miaka zaidi ya furaha Upendo wa kweli, urafiki na ndoa yenye Amani. Nakupenda. KHERI YA SIKU YA KUZALIWA MALKIA WANGU” alisema.

Esther Musila na mumewe Guardian Angel
Image: INSTAGRAM// ESTHER MUSILA

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Kenya Peter Omwaka almaarufu Guardian Angel amemsherehekea mkewe Esther Musila mnamo siku yake ya kuzaliwa.

Bi Musila ametimiza miaka 54 leo, Mei 25 na Guardian Angel ametumia siku hiyo kuzungumzia athari nzuri ambazo mama huyo wa watoto watatu wakubwa ameleta katika maisha yake katika miaka minne iliyopita ambayo wamekuwa pamoja.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ameelezea safari yake na Bi Musila kuwa ya ajabu na kutakia ndoa yao maendeleo mazuri pamoja upendo, urafiki na amani tele.

“Asante Mungu kwa kunipa zawadi nzuri. Asante mpenzi wangu. Asante kwa kuwa baraka kwa Maisha yangu. Miaka 4 ambayo nimeshiriki nawe malkia wangu imekuwa ya ajabu,” Guardian Angel alisema kupitia Instagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha ya kumbukumbu yake na mkewe ambayo ilichukuliwa wakati wa harusi yao iliyofanyika Januari 2022.

"Cheers kwa miaka zaidi ya furaha Upendo wa kweli, urafiki na ndoa yenye Amani. Nakupenda. KHERI YA SIKU YA KUZALIWA MALKIA WANGU” aliongeza.

Huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa,Bi Musila alimshukuru mumewe Guardian Angel kwa kuwa sehemu ya maisha yake katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Musila alieleza furaha yake na kuridhika kwake kwa kuwa na mwimbaji huyo wa nyimbo za injili na akasifu upendo ambao amempa tangu walipokutana.

“Mume wangu, asante mpenzi wangu, kwa kupendezesha maisha yangu na uwepo wako mzuri, kwa kuongeza kipimo tamu cha roho yako kwa uwepo wangu.

Hii ni siku yangu ya 4 ya kuzaliwa ambayo ninapata kusherehekea na wewe. Kila moja yao imekuwa ya kukumbukwa zaidi na maalum.

‘Kuwa na wewe katika maisha yangu kumenifanya kuwa mtu bora zaidi. Ninamshukuru Mwenyezi kila siku kwa kukuleta katika maisha yangu. Kwa kutembea safari hii ya maisha yangu na mimi, singetamani mtu mwingine yeyote. Jinsi unavyonipenda, unanifanya nihisi kupendwa na kutunzwa na kulindwa,” aliandika

“Asante kwa kunikumbusha jinsi mahaba yalivyo.😋😋 Nakupenda sana. Asante kwa Kuja G.❤❤❤," aliongeza.

Guardian Angel na mke wake Esther Musila walifunga ndoa katika harusi ya faragha iliyofanyika Januari 4, 2022. Walikuwa wamechumbiana tangu 2020.