logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nimepewa talaka mara 3- Amber Ray afunguka kuhusu ndoa zilizovunjika

Amber Ray alibainisha kuwa ndoa zinapaswa kufafanuliwa kwa mapenzi na sio vyeti vya ndoa.

image
na Radio Jambo

Habari25 May 2024 - 11:47

Muhtasari


•Alifichua kuwa mume wake tayari amemvisha pete ya uchumba lakini akabainisha kuwa kwa sasa hajali sana kuhusu ndoa rasmi.

•Bi Amber Ray aliwahi kuwa kwenye ndoa na mfanyabiashara Jimal Rohosafi, mbunge wa sasa na baba wa mtoto wake wa kwanza.

Mwanasosholaiti mashuhuri wa Kenya Faith Makau almaarufu Amber Ray amezungumza kuhusu mipango ya ndoa rasmi na mumewe Kennedy Rapudo.

Akiongea kwenye mahojiano na Betty Kyallo kwenye kipindi cha This Friday with Betty, mama huyo wa watoto wawili alibainisha kuwa ameridhishwa na hali ya ndoa yao.

Alifichua kuwa mume wake tayari amemvisha pete ya uchumba lakini akabainisha kuwa kwa sasa hajali sana kuhusu ndoa rasmi na mfanyibiashara huyo tajiri.

“Ashaweka pete, lakini ile ya harusi.. unajua mahali tumefika imekuwa miaka mitatu tayari. Sasa saa hii ata siwezi uliza harusi juu siwezi kujua kama amebadilisha mawazo,” Amber Ray alisema.

Mwanasosholaiti huyo ambaye maisha yake yamejawa na drama nyingi alibainisha kuwa ndoa zenye mafanikio zinapaswa kufafanuliwa kwa mapenzi na sio vyeti vya ndoa.

Ilikuwa wakati akizungumza kuhusu jinsi wa sherehe ya harusi isiyo ya muhimu sana ambapo alifichua kwamba tayari amepewa talaka mara tatu.

“Nilipo sasa hivi, nina furaha sana. Linapokuja suala la ndoa, ni poa inapokuja suala la uhakikisho. Lakini nahisi watu wawili wanapaswa kuwa pamoja kwa sababu ya mapenzi, sio kwa sababu ya cheti ama sijui nini, kwa sababu mimi nimepewa talaka mara tatu, ebu tafakari,” alisema.

Aliendelea, “Yaani mambo ambayo nimepitia katika maisha yangu, Sikuwa kufikiria hata katika ndoto zangu zisizo za kawaida kabisa kwamba nitapitia mambo hayo. Tunapanga, lakini Mungu ana mipango yake mwenyewe."

Kuhusu iwapo watu watarajie harusi kati yake na Rapudo hivi karibuni, Amber Ray alibainisha kuwa mume wake ndiye mtu sahihi wa kujibu swali hilo.

Bi Amber Ray aliwahi kuwa kwenye ndoa na mfanyabiashara Jimal Rohosafi, mbunge wa sasa na baba wa mtoto wake wa kwanza.

Mwanasosholaiti huyo mrembo kwa sasa ameolewa na Kennedy Rapudo na kwa pamoja wana mtoto mmoja anayeitwa Afrikanah Rapudo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved