"Umefungwa kwangu maisha yote!" Nadia amwambia Arrow Boy, afichua nyakati anazomkasirikia

Nadia amemsherehekea mpenzi wake na mzazi mwenzake Arrow Boy anapoadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Muhtasari

•Nadia alimuonya mpenziwe kuhusu mabadiliko ya mara kwa mara ya hisia zake akibainisha kwa kawaida yeye huwa mkali haswa kipindi cha hedhi.

•Huku akijisherehekea mnamo siku yake ya kuzaliwa, Arrow Bwoy kwa upande wake alibainisha kuwa umbali aliofikia maishani ni Mungu.

Nadia Mukami na Arrow Bwoy
Image: HISANI

Malkia wa muziki wa Kenya Nadia Mukami amemsherehekea mpenzi wake na mzazi mwenzake Arrow Boy anapoadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Wakati akisherehekea baba wa mtoto wake kwenye Instagram, mwanamuziki huyo mrembo alimwambia mpenziwe kuwa wamefungwa pamoja kwa maisha yao yote.

Pia alichukua fursa kumuonya kuhusu mabadiliko ya mara kwa mara ya hisia zake akibainisha kuwa kwa kawaida yeye huwa mkali haswa kipindi cha hedhi.

“Heri ya siku ya kuzaliwa Baba watoto! Umekwama nami kwa maisha! Katika nyakati nzuri na mbaya! Hasa hiyo kaperiod wakati wa hedhi na siwezi kujua kwa nini nina hasira na wewe! Hata mimi hutengeneza vitu kichwani mwangu 😄Hiloo pia😄 Ni mimi tu ama wanawake wenzangu?,” Nadia alimwandikia mpenziwe siku ya Jumapili.

Huku akijisherehekea mnamo siku yake ya kuzaliwa, Arrow Bwoy kwa upande wake alibainisha kuwa umbali aliofikia maishani ni Mungu.

Wanamuziki hao wawili wamekuwa wakichumbiana kwa takriban miaka minne iliyopita na hata wana mtoto mmoja mvulana pamoja, Haseeb Kai ambaye alizaliwa mapema mwaka wa 2022.

Safari ya mapenzi ya wawili hao hata hivyo haijawa laini kwani katika siku za nyuma waliwahi kuachana nakurudiana. Pia kwa bahati mbaya walipoteza ambaye angekuwa mtoto wao wa kwanza kama bado hajazaliwa mwaka 2021.

Mwaka wa 2022, Nadia alifichua kwamba aliamua kuzama kwenye mahusiano na Arrow Bwoy kwa vile alivyomtunza kama binti wao kifalme.

Mwimbaji huyo alikiri kuwa wamepitia mengi pamoja huku akisema anatazamia kuishi maisha yake yote pamoja na msanii huyo mwenzake.

"Nilisema Ndiyo kwa mpenzi wa maisha yangu Arrow Bwoy. Nilikupenda kwa sababu ya jinsi ulivyokuwa unanichukulia kama binti wa kifalme. Una Moyo wa Kustaajabisha zaidi. Moyo wako ni safi na siwezi kungoja kuishi maisha yangu yote na wewe. Tumepigana vita vingi sana pamoja. Watu wanaona msanii, mvulana mbaya. Ninaona mtu wa familia anayewajibika. Mwanangu ana bahati ya kuwa na wewe kama baba. Amebarikiwa sana. Nadhani wanaume wa familia yako wamelelewa vizuri kwa vile wanavyojibeba. Mungu ambariki mama yako.  Hata katika Maisha Yanayofuata, bado nataka kuwa nawe. Nakupenda Ali Etale. Malengo na ndoto zetu mwaka huu zinaanza Kudhihirika. Nataka kuwa tajiri na wewe ," Nadia alisema.

Mahusiano ya Arrow Bwoy na Nadia yalikuja kujikana hadharani mwaka wa 2021.