Sikuzaliwa kuruka kutoka kitanda kimoja hadi kingine - Akothee azungumzia kuwa na wanaume wengi

Akothee alibainisha kwamba sio rahisi kwake kutoka nje ya mahusiano yake kwani anaweza kushikwa kirahisi.

Muhtasari

•Mama huyo wa watoto watano alibainisha kuwa kawaida huwa anaangazia uhusiano mmoja na huwa mwaminifu kwa mpenzi wake.

•Alisema kwamba huwa anapigania mahusiano yake hadi anachoka na kuyaacha.

Esther Akoth almaarufu Akothee
Image: HISANI

Mwanamuziki na mjasiriamali maarufu wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee ameweka wazi kwamba huwa hachezi karata nje katika mahusiano yake.

Katika taarifa yake ya Jumanne asubuhi, mama huyo wa watoto watano alibainisha kuwa yeye kawaida huwa anaangazia uhusiano mmoja na huwa mwaminifu kwa mpenzi wake.

Alisema kwamba huwa anapigania mahusiano yake hadi anachoka na kuyaacha, na kuacha nafasi ya mwanaume mwingine anayeweza kuwa tayari kumchukua.

"Sikuzaliwa mwanamke ambaye anaruka kutoka kitanda kimoja hadi kingine. Siku zote ninazingatia uhusiano mmoja. Sijui ku’cheat,” Akothee alisema kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Mwimbaji huyo aliendelea kwa kusema, “Nelly anaweza kukuambia napigania mahusiano yangu haijalishi yameharibika kiasi gani. Lakini mikono yangu itakapochoka kushikilia, nitaiacha na kuizungusha kwa uhuru, ikiwa tu mwanaume mwingine anataka kuishikilia. Siruhusu zaidi ya mwanaume mmoja kunishika mikono, huwa nahisi kukosa hewa kichwa changu kiko bize kukurekebisha mahali fulani. Ni moja baada ya nyingine.”

Akothee alibainisha kwamba sio rahisi kwake kutoka nje ya mahusiano yake kwani anaweza kushikwa kirahisi.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alitoa maoni hayo alipokuwa akiwashauri watu dhidi ya kuiga maisha yake bila kufuata hadithi yake.

“Mimi, Esther Akoth Kokeyo, nitafika mbinguni nikiwa nimechoka, na malaika watanipokea nikiwa mwembamba kama kipande cha karatasi. 😆😆😆😆 Somo kwa mwanamke, Kuwa mkarimu kwako mwenyewe kusema Hapana bila kujisikia hatia,” alisema.

Inaaminika kuwa kwa sasa Akothee anachumbiana na meneja wake Nelson Oyugi almaarufu Nelly Oaks. Wawili hao walirudiana muda baada ya mama huyo wa watoto watano kutengana na mzungu Denis Schweizer almaarufu Omosh ambaye alikuwa amefunga naye ndoa rasmi Aprili mwaka jana.

Takriban miezi mitano iliyopita, mwimbaji huyo wa miaka 43 alionekana kuthibitisha kufufuka kwa mahusiano yake na meneja wake wa muda mrefu Nelly Oaks katika kipindi cha moja kwa moja cha hivi majuzi kwenye mtandao wa TikTok.

Katika kipindi hicho ambacho alikuwa akiwahutubia mashabiki wake Nelly Oaks akimwandalia chakula maalum jikoni, Akothee alisikika akimwita meneja huyo wake ‘babe’ mara kadhaa, jina ambalo hutumika sana sana  wapenzi.

Nelly Oaks pia alisikika akimtaja Akothee kuwa mtu maalum kwake huku wawili hao wakishiriki matukio ya kimapenzi kwenye kamera.