Jamaa anayejiona 'handsome' Kenya adai wasichana wanaomtaka wamezidi

Kuwa the most handsome guy in Kenya ni kichaa, nimechoka na wasichana, nimechoka!

Muhtasari

•Pretty Boi Raymar alidai kuwa sura yake ilimfanya kuwa anayependeza hapa nchini.

•Kijana anayedai kuwa na sura nzuri zaidi nchini Kenya alichapisha video akilalamika kuhusu wanawake wanaomfuata kwa wingi.

Prettyboi raymar

Mwanaume anayesema kuwa ni yeye  yuko na sura nzuri zaidi nchini Kenya, Pretty Boi Raymar, sasa anasema wasichana wanamfuata kila mahali.

Katika video, Raymar anaomba kuachwa peke yake, akisema amechoshwa na umakini anaopata kutoka kwa wanawake.

Raymar alifoka, akisema mara nyingi alikimbia wasichana ambao walimvutiwa na yeye na kudai kuachwa aishi maisha yake.

Hata hivyo, aliendelea na kusema kuwa anaelewa kwamba yeye ni handsome, lakini Wakenya wanapaswa kuacha kumzonga kuhusu urembo wake.

“Kuwa the most handsome guy in Kenya ni kichaa, nimechoka na wasichana, nimechoka! naomba muache kunitafuta.

 Wakenya niacheni nimechoka najua mimi ni handsome lakini naomba muache kukimbizana na mimi.

Wakijibu kauli hiyo, baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walisifu imani yake. Wengine, hata hivyo, walisema alikuwa akisumbuliwa na kutafuta umaarufu mtandaoni.

Patani Musa:

"Handsome who, handsome wapi, handsome vipi, handsome ipi?"

Djslimbkenya:

"They are chasing you, not running after you!"

Saji Made:

"Seems he doesn’t know the meaning of handsome."

Alckaraz Dlopez:

"I think this what we call self-denial."

Aww2615:

"It's nice to see an African proud of his skin tone."

Norahngala:

"This is the kind of delulu I aspire to have!"

Sarah:

"God have mercy upon us."