Hisia mseto baada ya Miracle Baby kutangaza kutawazwa kuwa mchungaji

“Wakati wowote ninataka kuongea mambo ya Mungu nikuwe nikilivaa na tunatumikia tukiwa pamoja,” alisema.

Muhtasari

• "Nimeidhinishwa kuwa mchungaji naye mtume wa Mungu John Paul," alitangaza.

•Miracle Baby amekuwa akipitia matatizo kadhaa hasa kulingana na afya yake ambapo mwaka wa 2018.

MIRACLE BABY
Peter Mwangi almaarufu Miracle Baby akiwa hospitalini MIRACLE BABY
Image: HISANI

Aliyekuwa mwanamuzi wa nyimbo za Gengetone wa kundi la SAILORS’ GANG, Peter Mwangi almaarufu Miracle Baby  aliamua kubadili miendendo na kuamua kumtumikia Mwenyezi Mungu kwa kuwa mchungaji wake.

Kauli hii ilipokelewa na  wengi kwa hisia mseto mitandaoni kwani wengi hawakuwa wametarajia msanii huyo maarufu wa nyimbo za Gengetone angebadili na kuwa mchungaji.

“Amina! Wakati mwingine inakufikisha mahali ambapo unamshukuru Jalali  mahali amekutoa... tunaweza kuwa hatuelewi,”aliandika Raff Mshairi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

“Mungu anawatumia watu wa kawaida katika kufanya mipango Yake ya kimaajabu.  Mungu akutumie kwa njia hodari zaidi,”aliandikisha Leila Ciku kwa ukurasa wa Instagram.

Miracle Baby amekuwa akipitia matatizo kadhaa hasa kulingana na afya yake ambapo mwaka wa 2018 alitambuliwa kuwa na matatizo yanayojihusisha na tumbo kisha kufanyiwa upasuaji maalum mwaka huo.

“My good names are Pastor Peter Mwangi  i’m a Miracle baby as you know me,” alisema kisha akafuatia na kusali.

“Naam, nimetawazwa kuwa mchungaji naye mtume wa Mungu John Paul. Nilipewa hii!” Alisema huku akionyesha mkufu wa msalaba aliokuwa amevaa shingoni.

“Wakati wowote ninataka kuongea mambo ya Mungu  nikuwe nikilivaa na tunatumikia tukiwa pamoja,” aliendeleza uneni wake Miracle Baby.“Tazama, mimi ni kiumbe kipya; ya kale yamepita. Sasa nikumtumikia Mungu  bila kurudi nyuma,”alizidi kusema Miracle baby.

Yakini mashabiki wengi walipigwa na butwaa isiyo na kifani huku wengine wakimpongeza Peter Mwangi kwa juhudi ya kuamua kujitoa kutoka kwenye anasa za dunia na kujinadhifisha kuwa kiumbe kipya namna alivyosema huku wengine wakishindwa kuamini kauli hiyohiyo.

“Anyoe nywele tuamini,” aliandika Sabato Sautiyaground pale Instagram.

“The spirit of laughter !” aliandika Stadees1986.

Naam, huenda majaribu aliyopitia Miracle Baby ndiyo chanzo kikuu cha yeye kubadili mienendo yake kulingana na kauli za baadhi ya wakenya huku wengine wakinena kuwa pengine ameamua kutumia dini kujinufaisha ama kunufaisha waumini wa Kristo ila wengi wanasema muda ndio utakao tupa jibu mwafaka ya kung'amua ukweli katika kauli hizi mbili