Siku ya Jumapili, Juni 2, mke wa mwimbaji wa nyimbo za injili Guardian Angel, Esther Musila alimsherehekea mwanawe Glenn Naibei almaarufu Jamal alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Jamal ambaye ni wa mwisho kati ya watoto watatu wa Bi Musila na marehemu mumewe aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya 26 na mamake alitumia siku hiyo kueleza upendo wake kwake.
Huku akimsherehekea mwanawe, mhasibu huyo mwenye umri wa miaka 54 alimuombea furaha na afya njema. Pia alitumia fursa hiyo kumtia moyo Jamal na kumtakia ujasiri na dhamira anapopambana na maisha.
"Heri ya miaka 26 kwako, mwanangu @__jama1. Nakuombea kwa Mungu akupe afya njema na furaha maishani. Unaposherehekea siku yako maalum, ninakutakia furaha B,” Esther Musila alimwandikia mwanawe Jamal kupitia mtandao wa Instagram.
Aliongeza, "Siku hii ya kuzaliwa iwe ukumbusho wa kila wakati kujitahidi kupanda mlima wowote unaosimama kwenye njia yako, na Mungu Mwenyezi aongoze hatua zako. Nakutakia ujasiri na dhamira, na uwe na mwaka mzuri na maisha matukufu mbeleni. Heri ya kuzaliwa. nakupenda ♥️.”
Wakati akijibu ujumbe huo mzuri kutoka kwa mama yake, Jamal alimshukuru na kukiri kwamba asingesherehekea siku hiyo ikiwa sio yeye.
“Asante mama, siku hii isingeweza kutokea bila wewe. Baraka na upendo wako unasikika kweli. Mungu akubariki,” aliandika Jamal.
Bi Musila ni mama wa watoto watatu wazima. Watoto wake wamejaribu kujitenga na maisha ya watu mashuhuri na wanajulikana tu kwa majina Gilda Naibei, Glenn Naibei (Jamal), na Ki
Jamal ambaye aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa mnamo Jumapili ndiye mtoto wa mwisho kati ya watoto wa Bi Musila.