Mpenzi wa Mulamwah, Ruth K afichua sababu ya kutoweka mtandaoni

Ruth katika video mpya kwenye YouTube yake, alieleza huku akiomba msamaha kwa kutoweka

Muhtasari

•Ruth alirejea siku chache zilizopita, jambo lililowafurahisha mashabiki wake ambao walikuwa wakihoji kutoweka kwake.

•Alishukuru mashabiki wake wakubwa kwa kusubiri kwa subira kurudi kwake.

Image: INSTAGRAM// RUTH K

Mzazi mwenza wa Mulamwah, Ruth K amekosekana  mtandaoni kwa wiki tatu. Alirejea siku chache zilizopita, jambo lililowafurahisha mashabiki wake ambao walikuwa wakihoji kutoweka kwake.

Ruth katika video mpya kwenye YouTube yake, alieleza huku akiomba msamaha kwa kutoweka.

"Si mmenitafuta," alianza kwa kubainisha wasiwasi kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake.

Aliongeza kuwa alipokea jumbe nyingi za kibinafsi zikitafuta majibu.

"DM yangu ilikuwa full, are you okay, bestie we missed you bestie aki rudi."

Sasa anafichua kichocheo kipya, kwani mashabiki wake walitoa maoni kwa furaha kuhusu mwonekano wake mpya. Alionekana kupendekeza kwamba alikuwa Kitale akifurahia maisha ya utulivu.

"Niko hapa Nimekuja na miguu yote machakula za Kitale, makuku ma ugali zimenipee energy."

Alishukuru mashabiki wake wakubwa kwa kusubiri kwa subira kurudi kwake.

"Hata hivyo, watu wangu nilikuwa nimewakosa. Kwa wale ambao wamekuwa wakinichunguza, 'Asante.' Huko Instagram tulikuwa tuna chat."

Mama huyo wa mtoto mmoja hata alisema mapumziko kutoka kwa mitandao ya kijamii yamemfanya aongeze uzito, akipata familia,

"Nilijipea kidogo break. Kitale was good, I enjoyed, nili catch up, nimeongeza, mnacheki? Nimongeza, nilikuwa nalishwa kweli...mother in law, ma shemeji, ma cousin, ai, I want to go back."