Mwafrika afukuzwa Ulaya kwa kutumia link ya ibada ya maombi kwa rafiki Mzungu

Jamaa huyo alieleza kwamba Visa ake ilibatilishwa na kutakiwa kuondoka saa chache baada ya kumtumia rafiki yake mzungu link ya kujiunga na ibada ya maombi ya kimtandaoni.

Muhtasari

• Alifichua kuwa Mnigeria alifukuzwa baada ya Cheti cha Udhamini cha mtu huyo (CoS) kubatilishwa kwa kutuma link ya NSPPD.

Image: BBC

Jamaa mmoja Mwafirka Raia wa Nigeria anaripotiwa kufukuzwa kutoka moja ya nchi ya Ulaya aliyokwenda kutafuta maisha kutokana na kile alichokitaja kuwa ni kumtumia rafikiye mwenye asili ya Ulaya link ya kushiriki maitka ibada ya maombi ya kanisa yake mtandaoni.

 Kupitia jukwaa la X, awali ikijulikana kama Twitter, jamaa huyo kwa jina la @Morris_Monye alishiriki kuwa hilo lilimtokea rafiki yake raia wa Nigeria saa chache baada ya kumtumia rafikiye mwenye asili ya Ulaya link hiyo na baadae kupokea taarifa kwamba visa yake ya kuendelea kuishi katka taifa hilo la Ulaya imefutiliwa mbali na hana kibali cha kuendelea kuishi nchini humo.

Alifichua kuwa Mnigeria alifukuzwa baada ya Cheti cha Udhamini cha mtu huyo (CoS) kubatilishwa kwa kutuma link ya NSPPD.

NSPPD inawakilisha Sala na Matamko ya Kinabii ya Msimu Mpya, ambayo ni mkutano wa maombi ya kidijitali mtandaoni ulioandaliwa na Mchungaji Jerry Eze, mwanzilishi wa Streams of Joy International Church nchini Nigeria.

"Unatuma NSPDD kwa mzungu mwenzako kisha wanabatilisha COS yako na wewe kurudishwa Nigeria. Loseguard,” chapisho lake lilisoma.

Chapisho hilo lilivutia maoni mbalimbali kutoka kwa watu waliojimwaya kutoa upande wao wa simulizi jinsi walijipata katika hatari ya kufukuzwa katika mataifa ya kigeni kutokana na baadhi ya vitu walivyovifanya bila kujua athari zake.

Tazama chapisho hilo hapa na jinsi watu walitoa maoni yao’