Jamaa akiri kwenye video kutoka kimapenzi na mke wa mwanaume mwenza, “Naomba nisishikwe!”

Jamaa huyo ali'share video akiwa kwenye nyumba ya mwanamke huyo kando ya kitanda akiwa bila shati na kukiri kwamba anatambua mwanamke huyo ni mke wa mtu lakini anaomba asije kushikwa na mume wake.

Muhtasari

• Mtu huyo asiyejulikana alikiri kwamba anatambua kuwa anachofanya ni mchezo hatari sana ambao unaweza kumgharimu sana.

• Walakini, aliomba asishikwe na mume wake au mtu mwingine yeyote.

Mwanaume mmoja mwenye umri wa makamo amewashangaza wengi baada ya kupakia video akikiri kwamba anatoka kimapenzi na mke wa mtu.

Jamaa huyo aliwashangaza wengi kwa kueleza kwamba hata katika video hiyo, alikuwa katika nyumba ya mwanamke huyo licha ya kutambua kuwa ni mke wa mtu, lakini akasema kwamba kila mara anapoingia kwenye nyumba hiyo, huomba asiwahi kuja kushikwa na mume mwenye nyumba.

Mtu huyo asiyejulikana alikiri kwamba anatambua kuwa anachofanya ni mchezo hatari sana ambao unaweza kumgharimu sana.

Walakini, aliomba asishikwe na mume wake au mtu mwingine yeyote.

Mtu huyo alisema kwamba ikiwa, hatimaye, atakapomatwa, watu hawapaswi kumpiga, lakini kumkabidhi kwa polisi.

“Hiki kitu ninachokifanya nifikishwe polisi siku nikikamatwa,” alisema.

Alishiriki video yake akiwa katika nyumba ya mwanamke huyo na kitanda kikionekana kutawanyika kutokana na shughuli.

Angalia maoni yaliyofuata ...

thriftwearbybellz alisema: "ni wanaume wachache tu wanaofaa kwa nchi hii"

estherwhytebassey alisema: “Unawezaje hata kumruhusu mtu mwenye midomo na meno ya aina hii alale nawe😭”

chinonso_anusionwu alitoa maoni: "Amini mitandao ya kijamii kwa hatari yako mwenyewe, hii inaweza kuwa nyumba na kitanda chake 🤣"

amyxious_bubz aliandika: “Ona mtu mume, kaka na baba. aibu aibu 😔"

mzz_vikky’ alitoa maoni yake: “Kila siku ni ya mwizi siku moja ni ya mwenye nayo kufurahia inapodumu”

Tazama video hiyo hapa;