Akina mama waandamana kulalamikia ongezeko la kuibiwa wanaume na mipango ya kando

Moja ya bango walilokuwa wameshika lilisomeka; “Tumechoka. Wasichana wasio na waume tafadhali waache waume wa wenyewe ili warudi kwa wake zao na watoto wao.”

Muhtasari

•“Tunataka mwisho kwa kunyakuliwa kwa wanaume, ikiwa tutakukamata na mwanamume wa mwenyewe, nitakuanika mitandaoni,” kiongozi wa maandamano hayo alisema.

Wanawake waandamana kulalamikia kuibiwa wanaume
Wanawake waandamana kulalamikia kuibiwa wanaume

Baadhi ya wanawake walioolewa wamezua gumzo mitandaoni huku wakitoka nje kupinga kasi ya kutisha ya unyakuzi wa waume unaoendelea.

Video hiyo inadaiwa kurekodiwa katika soko moja katika jimbo la Asaba nchini Nigeria na makumi ya wanawake wanaodaiwa kuwa katika ndoa walionekana wakiandamana na mabango yenye jumbe za kuelezea mfadhaiko wao dhidi ya ongezeko la ‘mipango ya kando’ kuwanyakua wanaume wao.

Katika jumbe kwenye mabango yao, akina mama hao walionekana wakijiburuza na kujitupa sakafuni kwenye lami wakidai kwamba ongezeko la wanawake wasio na wanaume kuwachukulia wanaume wao limesababisha wanaume wengi kuishia kutowajibika katika familia zao, kwani mara nyingi rasilimali nyingi huishia midomoni mwa michepuko na familia kusalia kutelekezwa.

Moja ya bango walilokuwa wameshika lilisomeka; “Tumechoka. Wasichana wasio na waume tafadhali waache waume wa wenyewe ili warudi kwa wake zao na watoto wao.”

Waliapa kuwafichua wanawake wasio na waume ikiwa watawakamata na waume zao.

“Tunataka mwisho kwa kunyakuliwa kwa wanaume, ikiwa tutakukamata na mwanamume wa mwenyewe, nitakuanika mitandaoni,” kiongozi wa maandamano hayo alisema.

Video hiyo iliyochapishwa katika jukwaa la X ilivutia maoni kinzani na haya hapa ni baadhi ya maoni yenye mvuto;

“Baada ya kuwafukuza waume zao wenye tabia mbaya, wanawalaumu michepuko kuwa anawafanyia kazi zao 🤣” Chaxton alisema.

“Kumbatia ndoa ya wanawake wengi na mfurahie maisha yenu,” mwingine aliwaambia.

“Dawa pekee ya kumtunza mume ni kumtendea mema na kujitiisha chini ya ukichwa wake katika ndoa yenu. Mara tu nyumba inapokuwa na joto sana kwake, wasichana wengine watampa joto.”Jeff Onyedili.

Tazama video hapa;