logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize na Diamond wafufua bifu, wabishana kuhusu nani mkali

Huku akionekana kumjibu bosi huyo wake wa zamani WCB, Konde Boy alichapisha chati mbili zilizomuonyesha akiongoza.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani05 July 2024 - 07:55

Muhtasari


  • •Walichapisha machapisho kwenye Instagram ambayo yalionekana kuwa mashambulizi yasiyo ya moja kwa moja dhidi ya kila mmoja wao.
  • •Huku akionekana kumjibu bosi huyo wake wa zamani WCB, Konde Boy alichapisha chati mbili zilizomuonyesha akiongoza.
katika picha ya maktaba.

Mastaa wa Bongofleva, Harmonize wa Konde Music Worldwide na Diamond Platnumz wa WCB wameonekana kurudi katika kuzozana hadharani.

Siku ya Alhamisi, wasanii hao ambao mara nyingi huchukuliwa kuwa wanamuziki wakubwa zaidi nchini Tanzania walichapisha machapisho kwenye mtandao wa Instagram ambayo yalionekana kuwa mashambulizi yasiyo ya moja kwa moja dhidi ya kila mmoja wao.

Diamond Platnumz ndiye aliyeanza mashambulizi hayo kwa kuchapisha screenshot ya chati ikimuonyesha kama mwanamuziki wa Tanzania ambaye alitazamwa zaidi kwenye YouTube mwezi wa Juni. 

“Simba na wanawe,” Diamond aliandika chini ya chati hiyo aliyoichapisha.

Katika chati hiyo, bosi huyo wa WCB alitazamwa na watazamaji 33.7m mnamo mwezi Juni, Rayvanny alikuwa na watazamaji 23.1m, Zuchu alishika nafasi ya tatu akiwa na watazamaji milioni 13.7, Mbosso alikuwa na views milioni 11.6 huku Harmonize akishika nafasi ya 5 akiwa na watazamaji milioni 11.

Huku akionekana kumjibu bosi huyo wake wa zamani WCB, Konde Boy alichapisha chati mbili zilizomuonyesha akiongoza.

“Hawawezi kupost hii!! Ni wakati wa Ibraah hata hivyo,” Harmonize aliandika kwenye chati ya wasanii bora katika wiki inayoanza Juni 21-Juni 27, 2024.

Bosi huyo wa Kondegang aliongoza orodha hiyo, huku Diamond Platnumz akifuatiwa na Rayvanny na Zuchu wakishika nafasi ya tatu na ya nne.

Chati ya pili aliyochapisha ilionyesha orodha ya video bora za muziki katika siku moja Juni 29, 2024 ambapo wimbo wake na Rayvanny ‘Sensema’ ulioongoza siku hiyo.

"Uko wapi baba," aliandika.

Wimbo ‘Siji’ wa Zuchu, Binadamu wa Kontawa na Disconnect wa Harmonize zilifuata kwa njia mfululizo kulingana na chati.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved