Wanandoa washerehekea kupata mapacha baada ya kusubiri kwa miaka 26!

Mwanamke huyo pia alimpongeza mumewe kwa kuwa na ujasiri wa kuwa na subira kwa kipindi chote hicho pasi na kuenda nje ya ndoa au kukata tamaa na ndoa na yeye.

Wanandoa kutoka wamevutia jumbe za pongezi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusimulia safari yao ya jinsi walilazimika kusubiri kwa hadi miaka 26 kabla ya kupata mtoto.

Wanandoa hao, mke na mumewe walipakia video akiwa na ujauzito na baadae kufichua kwamba alibarikiwa na watoto mapacha, ikiwa ni baada ya majaribio mengi ya kuitwa mama kufeli katika kipindi cha miaka 26.

 Hii ilifichuliwa katika video iliyotolewa kwenye jukwaa maarufu la media ya kijamii, TikTok, na mtumiaji.

Katika video hiyo, nyuso za wanandoa zinafunuliwa, zikiangaza kwa furaha. Muda si muda, mke anaonyeshwa akiwa amebeba watoto wawili wapya mikononi mwake.

Anaweza pia kuonekana kwenye video hiyo hiyo akicheza kwa furaha huku akikomesha ukosefu wake wa watoto baada ya zaidi ya miaka 26 ya ndoa.

Mwanamke huyo pia alimpongeza mumewe kwa kuwa na ujasiri wa kuwa na subira kwa kipindi chote hicho pasi na kuenda nje ya ndoa au kukata tamaa na ndoa na yeye.

“Ambacho Mungu hawezi akakifanya kwa maisha ya mja wake wala hakipo. Ninashukuru sana pongezi kwangu na mume wangu mpendwa,” mama huyo aliandika kwenye video hiyo aliyoinukuu kwa maandishi, “Mungu hatimaye ametenda baada ya miaka 26 kwenye ndoa, ametubariki na mapacha.”

Watu wengi waliokutana na video hiyo wamefurika sehemu ya maoni ya chapisho ili kusherehekea nao.

Hili hapa chapisho lenyewe kwa mtindo wa video;