Ushauri wa Corazon Kwamboka kwa wale walio kwenye mahusiano

‘Badilisha godoro hilo, limekusaidia katika mahusiano 8’

Muhtasari

•Akizungumza kupitia  Instagram yake, Kwamboka aliwashauri watu kubadilisha godoro ambayo kwa upande wake amesema imeshuhudia mahusiano nane juu yake.

•Amewataka Wakenya kufikiria kubadilisha magodoro yao au hata kuzitoa kwa madhumuni ya kisayansi.

CORAZON KWAMBOKA
Image: HISANI

Corazon Kwamboka, mwanasheria ambaye katika miaka ya hivi majuzi amejikita zaidi katika kuunda maudhui badala ya kufanya kazi kama wakili, ameonekana kuwashauri watu ambao wako kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Akizungumza kupitia  Instagram yake, Kwamboka aliwashauri watu kubadilisha godoro ambayo kwa upande wake amesema imeshuhudia mahusiano nane juu yake.

Amewataka Wakenya kufikiria kubadilisha magodoro yao au hata kuzitoa kwa madhumuni ya kisayansi.

Mama huyo wa watoto wawili alitania kuhusu baadhi ya watu kutumia godoro moja kupitia mahusiano mengi.

"Kuwakumbusha badilisha godoro hiyo au kuichangia kwa sayansi kwa bahati nzuri, imekuona kwa mahusiano 8," Corazon aliandika.

Corazon Kwamboka hivi majuzi ametangaza kuwa angetaka kurejea katika kazi ya uwakili kwa kuwa ilikuwa ndoto yake.

Akizungumza kwenye Instagram, Kwamboka aliangazia matukio ya hivi majuzi katika maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024.

"Nilipokuwa mdogo, nilikuwa na ndoto ya kuwa wakili wa kutetea wale wasioweza kujitetea wenyewe," alishiriki ujumbe Kwamboka.

"Licha ya kwamba njia yangu ilinipeleka sehemu nyingine kwa wakati huo, hamu ya kufanya mambo kwa utofauti ilibaki.

Kusoma sheria kwangu kulihamasishwa na waandishi kama John Grisham, haikuwa tu ndoto yangu pekee bali pia ya wazazi wangu," alieleza Kwamboka.

"Nia yangu iko wazi na bayana ;kutetea walio kwenye hatari, hasa kina mama wanaohitaji sauti," alitangaza Corazon.

"Misheni hii mpya inachochea roho yangu. Na cheti changu cha kufanya kazi kimeboreshwa, nipo tayari kuwatetea kwa moyo wangu wote wale wanaohitaji msaada zaidi." aliongezea.