Afisa Shakur azungumzia matukio baada ya kuandamana dhidi ya serikali

Kuhusu mswada wa sheria ya fedha, alisema amepokea maoni kutoka kwa askari wengine, huku wengine wakimuita shujaa.

Muhtasari

• Shakur alienda kwenye mitandao yake ya kijamii akisema kuwa alikuwa akifuatwa kila mahali alipoenda.

•Askari Shakur alimuambia mkewe haya kisha kuzima simu yake, akihofia kuwa ikiwa  aliwasiliana na  yeyote, wangepatikana.

Afisa Shakur akiandamana
Image: HISANI

Jackson Kuria Kihara Shakur  almaarufu Afisa Shakur amesimulia masaibu yake kufuatia kuwepo kwake wakati wa maandamano ya kupinga ushuru.

Shakur alienda kwenye mitandao ya kijamii akisema kuwa alikuwa akifuatwa kila mahali alipoenda. Alisema jambo hilo lilimfanya awasiliane na mkewe ili kumjulisha yafuatayo.

Askari Shakur alimuambia mkewe haya kisha kuzima simu yake, akihofia kuwa ikiwa  aliwasiliana na  yeyote, wangepatikana.

"Niliamua nizime simu nisicontact mtu yeyote juu nikicontact mtu yeyote, huyo mtu anaweza kufuatwa. Nikaamua tu niende incognito," alisema.

Askari Shakur alisema Jumamosi usiku, alikwenda Kikuyu, na nusura agongwe na gari.

Alisema alilala ndani ya gari kwa muda kabla ya kutafuta hifadhi katika eneo la Githurai 45 ambapo hakuweza kupatikana.

Alisema mkewe aliripoti kupotea kwake na wakili wake alifanya kazi ili kupata dhamana yake ya kutarajia.

Afisa Shakur alisema mkewe pia alifuatwa, na kusababisha kukamatwa kwake.Alidai alilazimishwa kufika hadi Ruiru na kisha kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kamiti.

"Tulikuwa pale kwa muda wa saa tatu tukisubiri kuachiliwa," alisema na kuongeza kuwa hakuwa amefungwa lakini hakuweza kutoroka.

Alisema karatasi ya mashtaka iliandikwa na kwamba kila kitu kimewekwa, pamoja na alama za vidole vyake. Askari Shakur alidai aliambiwa abaki kituoni akiambiwa kwamba hakuwa salama nje.

Alisema anasubiri kesi hiyo imalizike ndipo ajiuzulu, ambayo inachukua mwezi mmoja kukamilika.

Kuhusu muswada wa sheria ya fedha, alisema amepokea maoni kutoka kwa askari wengine, huku wengine wakimwita shujaa kwa kusimama.

“Lakini sasa hao wasee wananipersecute sana,” alisema.

Aliwashukuru waliompigania huku akiwataka Wakenya kutofanya mazungumzo hadi haki ipatikane kwa waliouawa wakati wa maandamano.

Askari Shakur alisema baada ya kujiuzulu anatarajia kurejea shuleni, akiomba wafadhili.