logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vera Sidika aapa kumficha baba wa mtoto wa tatu

Kwa sasa anaendelea kuwalea watoto wawili, wa kike na wa kiume, aliozaa na aliyekuwa mume wake Brown Mauzo.

image
na Samuel Maina

Burudani30 July 2024 - 09:08

Muhtasari


  • •Vera ameweka wazi kuwa umma hautawahi kumjua mzazi mwenzake ajaye, iwapo ataamua kupata mtoto mwingine katika siku zijazo.
  • •Kwa sasa anaendelea kuwalea watoto wawili, wa kike na wa kiume, aliozaa na aliyekuwa mume wake Brown Mauzo.
VERA SIDIKA

Mwanasosholaiti maarufu wa Kenya Vera Sidika ameweka wazi kuwa umma hautawahi kumjua mzazi mwenzake ajaye, iwapo ataamua kupata mtoto mwingine katika siku zijazo.

Katika taarifa kwenye ukurasa wake wa Instagram, mama huyo wa watoto wawili alisema kuwa atahakikisha kuwa utambulisho wa baba wa mtoto wake ajaye utasalia kuwa siri.

Alieleza kuwa hatua hiyo itazuia watu kuingilia mambo yake na kuzingatia mambo yao wenyewe.

"Ikiwa nitaamua kuwa na mtoto tena siku zijazo, hakuna mtu atakayemjua baba. Nyote itabidi mjifunze jinsi ya kuzingatia mambo yenu kwa kweli," Vera alisema Jumatatu jioni.

Hiki kinaweza kuwa kiashiria kwamba sosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 34 hajatupilia mbali uwezekano wa yeye kupata mtoto wa tatu katika siku za usoni.

Kwa sasa anaendelea kuwalea watoto wawili, wa kike na wa kiume, aliozaa na aliyekuwa mume wake Brown Mauzo, Wazazi wenza hao wawili hawapo pamoja tena.

Mapema mwaka huu, Vera alitangaza msimamo wake kuhusu mustakabali wa idadi ya watoto anaotarajia kuwapata katika siku zijazo.

Mama huyo wa watoto wawili kupitia ukurasa wake wa Instagram alionekana kutosheka na idadi ya wanawe kwa sasa huku akisema kwamba hana mpango wa kuongeza mtoto kwa angalau miaka 7 ijayo.

“Hakuna watoto Zaidi kwangu kwa angalau miaka 7 ijayo. Hapana,” Vera Sidika aliandika.

Kwenye ujumbe huo, Sidika aliongeza kwamba msimu ujao wa joto, kuna baadhi ya vitu ambavyo atahakikisha amevikwepa kabisa navyo ni kupata mimba, kuwa na huzuni na kufilisika.

“Vitu vinne ambavyo sitaki vinipate majira ya msimu wa joto ni kupata mimba, kufilisika, kuwa na huzuni na kupata mimba.”

Mwishoni mwa Agosti mwaka jana, Mauzo alitangaza kuwa yeye na Vera wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.

"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved