Maoni mseto baada ya Size 8 kutangaza kuvunjika kwa ndoa yake ya miaka 11

Size 8 alidokeza kuhusu kutengana kwake na DJ Mo kwa kutangaza kwamba anaanza safari yake ya kuwa single.

Muhtasari

•Tangazo hilo limezua mjadala mkubwa kwenye mitandao, wengi wakionekana kutoamini kuwa wasanii hao wawili wametengana.

•Baadhi ya watumiaji wa mtandao hata hivyo wanaonekana kushawishika kuhusu tangazo hilo, na wameendelea kutoa maoni.

Image: INSTAGRAM// SIZE 8 REBORN

Wakenya wengi wanaonekana kutoamini baada ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Linet Munyali almaarufu Size 8 kutangaza kuvunjika kwa ndoa yake ya miaka kumi na moja.

Siku ya Alhamisi, mama huyo wa watoto wawili alidokeza kuhusu kutengana kwake na mcheza santuri Samuel Muraya almaarufu DJ Mo kwa kutangaza kwamba anaanza safari yake ya useja.

Size 8 amekuwa kwenye ndoa na  DJ Mo kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita na wamebarikiwa na watoto wawili pamoja, msichana mmoja na msichana mmoja.

"Wakati mwingine ndoa hufanya kazi kwa neema ya Mungu, na wakati mwingine haifanyi kazi, lakini yote kwa Mungu bado yuko kwenye kiti cha enzi," Size 8 alisema kupitia Instagram.

Aliongeza, "Nimeolewa kwa miaka 11 na sasa ninaanza safari ya kuwa mseja. Lakini Mungu bado yuko kwenye kiti cha enzi, nakuabudu wewe Yaweh!"

Hata hivyo, mwanamuziki huyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu hali ya ndoa yake au sababu iliyosababisha yeye kutengana na mzazi mwenzake. DJ Mo kwa upande wake hajanena lolote kuhusu tangazo lililotolewa na mke wake.

Tangazo hilo limezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakionekana kutoamini kuwa wasanii hao wawili wametengana. Baadhi ya wanamtandao hata wamemshutumu mwimbaji huyo wa nyimbo za injili kwa kutafuta kiki na kudai kwamba anaweza kuwa anajiandaa kutoa wimbo.

Baadhi ya watumiaji wa mtandao hata hivyo wanaonekana kushawishika kuhusu tangazo hilo, na wameendelea kutoa maoni na majibu kuhusu maendeleo ya hivi majuzi.

Tazama maoni ya baadhi ya wanamtandao;

Njeri_gitau: Is clout chasing allowed in the bible?

Wahitotravels: This babe can’t leave the DJ, beat her or wonder around, she can’t.. this is a new song coming..

Kevoh_kinds_:" Sasa toa ngoma uache kutubeba kama kina bahati.

Waruguru_waweruu: Surely, if you knew how I always look up to your marriage, your break up will hurt me personally, nimegive up walai.

Gachugu_maggy: Some of us admire marriage because of you people, if it is clout, may it be from your mouth to God’s ears and if not, may peace be with you.

Bmayienda: Hata watumishi wa Mungu pia hutafuta kiki, wacheni kutuconfuse sisi wanakondoo.

Mapema mwaka huu, Size 8 alifichua kwamba aliwahi kutaka kugura ndoa yake na DJ Mo na hata akatafuta usaidizi wa wakili wa talaka.

Wakati akizungumza katika kipindi cha uhalisia kilichopeperushwa kwenye runinga ya TV 47, mama huyo wa watoto wawili alifichua kwamba alikuwa amepoteza matumaini katika ndoa yake kiasi cha kutaka kuivunja.

“Kilichofanyika, ilifika mahali nikawa sina matumaini, nikawa nimefika hatua ya kutorudi nyuma. Nadhani msongo wa mawazo pia ulianza. Kwa hivyo sikuwa nikifikiria sawa na sikuwa nikiona njia ya kutoka. Ndiyo maana niliamua kumwita wakili wa talaka,” Size 8 alisimulia.

Mwimbaji huyo alifichua kuwa baada ya kumweleza mwanasheria wa talaka kuhusu nia yake ya kuvunja ndoa yake, hata alimwelekeza aanze kutayarisha karatasi rasmi za hatua hiyo. Alisema kuwa alitaka kutenganishwa na mcheza santuri huyo na kuruhusiwa kwenda na watoto wao wawili.

Talaka hiyo hata hivyo haikuendelea baada ya mama huyo wa watoto wawili kuzungumza na mamake DJ Mo na pia kuhudhuria likizo ya mafunzo ambayoilimfanya apate hamu ya kuipa ndoa hiyo nafasi nyingine.

“Tuko karibu sana na mama yake. Aliniambia nimekasirika nisifanye mambo kwa haraka. Kisha mhubiri alikuwa ametaja likizo takriban wiki mbili kabla, ilikuwa imebaki mwezi hadi tarehe ya likizo. Nilisema, nitapatia ndoa yangu nafasi moja ya mwisho,” alisema.

Size 8 alisema baada ya kuhudhuria mafunzo hayo, alikubali kutulia na kutazama iwapo mume wake naye angekuwa tayari kuifanyia kazi ndoa yao.