Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize na sosholaiti Poshy Queen wanaonekana kutokuwa katika hali ya maelewano tena.
Mastaa hao wawili wa bongo ambao wamekuwa wakichumbiana kwa miezi kadhaa sasa wameripotiwa kuvunja uhusiano wao, huku wote wawili wakipeana vidokezo kwa ku-unfollow kila mmoja kwenye mitandao ya kijamii.
Uchunguzi wa kina kwenye majukwaa yao ya mitandao ya kijamii ya Instagram unaonyesha kuwa hawafuatilianii tena kama hapo awali. Haijabainika ni lini hasa waliacha kufuatana hivi majuzi lakini inaaminika kuwa ni punde baada ya kutofautiana.
Chanzo cha matukio ya hivi majuzi bado hakijajulikana kwa umma lakini kumekuwa na taarifa ambazo hazijaripotiwa kutoka Tanzania kuwa bosi huyo wa Kondegang alichukizwa na mpenzi wake huyo kuonekana kutaniania na mwanaume mwingine, tukio lililosababisha waachane.
“Kuna mwanaume alimmiminia Champagne Poshy wakati Harmonize anacheza muziki kule, wapo bize wanavibe pale. Ile ikaleta maneno, Harmonize hakupenda. Akauliza kwa nini anakumiminia Champagne, au anakutaka wewe kwa nini unamchekea. Harmonize akamwaga ile Champagne, wakakasirika ikatokea maneno ya watoto na kuvutana kidogo, wakachukuana wakaondoka,” alisema ripota wa Millard Ayo TV, Vido Vidox.
Aliongeza, “Za kudaiwa zinasema ndio hapo ikabidi Poshy na Harmonize wakazinguana. Poshy akaenda kwake, Harmonize akabaki kwake. Ilipokuja mitandaoni, wakakuta picha zimefutwa. Kila mmoja amefuta picha za mwingine. Alafu kila mmoja amemuunfollow mwenzie “
Wasanii hao wawili wa Tanzania wamekuwa wakichumbiana kwa takriban miezi minane sasa.
Habari kuhusu uchumba wao ziliibuka mapema mwaka huu, na kusababisha mijadala mingi na msisimko kwenye mitandao ya kijamii.
Mapema mwaka huu, Konde Boy alidokeza kuwa uhusiano wake mpya hauhusishi kuficha mambo yoyote akifichua kuwa mwanamke anayechumbiana naye huwa na simu yake wakati mwingine.
"Mwanaume mwaminifu ulimwenguni! Mpenzi wangu huenda na simu yangu ya rununu, tayari ana password ya simu yangu. Iwapo utapata jibu lisilo la kawaida, bado nina upendo nanyi nyote,” alisema Harmonize kupitia Instastories yake.
Mwanamuziki huyo alifichua kuwa alitaka kuchumbuina na mpenzi wake kitambo lakini uhusiano wao haukufaulu wakati huo kama walivyokusudia.
Aidha, aliendelea kutangaza kuwa sasa ametulia kwani mwanamke anayetoka naye sasa hivi atakuwa wa kudumu kwake.
“Hapa ndio mwisho wangu. Onyoo, hajawahi kutembea na yeyote ninayemjua. Mheshimu kama msichana wangu. Popote utakapomuona uache drama!” alisema