logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mchekeshaji Aunty Jemimah afichua kwa nini anaogopa ndoa

"Naona ndoa inakuja nakimbia, sipo tayari. Mtu mmoja ndani ya nyumba maisha yako yote? Ningechoka," alisema.

image
na Samuel Maina

Burudani11 August 2024 - 13:00

Muhtasari


  • •"Naona ndoa inakuja nakimbia, sipo tayari. Mtu mmoja ndani ya nyumba maisha yako yote? Ningechoka," alisema.

Mchekeshaji Aunty Jemimah amefichua kuwa anaogopa ndoa.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio cha humu nchini, Jemimah alisema anaogopa kuamka na mtu yule yule kila siku.

"Kama kuna kitu ninaogopa maishani mbali na umaskini na njaa ni ndoa.

Naona ndoa inakuja nakimbia, sipo tayari.

Mtu mmoja ndani ya nyumba maisha yako yote? Ningechoka.

Labda siku moja nitafika huko."

Jemimah anasema alizungumza na mpenzi wake kuhusu hili

"Mimi ni mkweli sana, nilipoanza kuchumbiana naye, nilimwambia nataka kwanza nipate watoto, niwe sawa kiuchumi na alikuwa sawa.

Amekomaa sana. Ikiwa ningekutana naye kabla ningeweza kuolewa."

Jemimah alipoteza mtoto wake wa kwanza kutokana na kisukari cha ujauzito.

Alilazimika kuwa induced akiwa na wiki 35 wakati wa ujauzito wake wa pili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved