logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akothee ajigamba kuhusu mafanikio ya bintiye wa miaka 24; Kazi nzuri, elimu, mume tajiri

Mama huyo wa watoto watano aliorodhesha mafanikio kadhaa ambayo bintiye amepata akiwa na umri wake wa miaka 24 tu.

image
na Samuel Maina

Burudani20 August 2024 - 12:37

Muhtasari


  • •Mama huyo wa watoto watano aliorodhesha mafanikio kadhaa ambayo bintiye amepata akiwa na umri wake wa miaka 24 tu.
  • •"Anachumbiana na mhandisi. Mume wake hivi majuzi alimnunulia gari, na anitumia pesa za kusaidia Foundation yangu," alisema.
ameonekana kujivunia baada ya bintiye Fancy Makadia kuchumbiwa na mpenziwe

Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee amemmiminia sifa tele binti yake wa tatu, Fancy Makadia.

Katika taarifa ya Jumanne, mama huyo wa watoto watano aliorodhesha mafanikio kadhaa ambayo bintiye amepata akiwa na umri wake wa miaka 24 tu.

Alibainisha kuwa mbali na kuwa anaendelea na shahada yake ya uzamili, Makadia ambaye kwa sasa anaishi Ufaransa pia anachumbiana na mwanaume tajiri, anafanya kazi nzuri na anaishi vizuri Ulaya.

"Usitegemee sana maisha yangu ya zamani, ndio msingi wa sasa wangu. Binti yangu wa mwisho Fancy Makadia ana umri wa miaka 24, akimaliza shahada yake ya uzamili mwaka huu, anafanya kazi na yuko imara Paris Ufaransa,” Akothee aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

Mwimbaji huyo alizungumza kuhusu jinsi mchumba wa bintiye alimnunulia gari hivi majuzi na hata jinsi anavyokutuma pesa kusaidia Akothee Foundation.

"Anachumbiana na mhandisi. Mume wake hivi majuzi alimnunulia gari, na anitumia pesa za kusaidia Foundation yangu. Sasa, una umri gani, na unafanya kazi gani? & mama yako yuko wapi? na umemfanyia nini?" alihoji.

Makadia ni mtoto wa tatu wa Akothee na wa mwisho akiwa na mumewe wa kwanza Jared Okello Otieno. Ameishi muda mwingi wa maisha yake ya ujana nchini Ufaransa.

Machi mwaka huu, Akothee alionekana kuwa mzazi mwenye fahari baada ya bintiye huyo kuchumbiwa na mpenzi wake Fairouz Vivian Ligali Ali.

Makadia na mpenzi wake walipeleka uhusiano wao katika hatua nyingine wakati walipokuwa likizoni kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Msichana huyo alionekana kujivunia sana kukubali ndoa na mpenzi wake na akabainisha amefurahishwa na ukurasa wao mpya.

"Nasema 'I do' kwa milele na rafiki yangu bora," Fancy Makadia aliandika chini ya video ya iliyomuonyesha mpenzi wake akimvisha pete kidoleni.

Pia alishiriki video nyingine iliyonyesha akijigamba na pete ambayo mpenzi wake aliweka kwenye kidole chake na katika sehemu ya maelezo, akamtambulisha Bw Fairouz kama mpenzi wake wa roho.

"Nimefurahi kuanza sura hii mpya na mwenzi wangu wa roho," aliandika.

Makumi ya wanamitandao ikiwa ni pamoja na mamake Akothee na dada zake Rue Baby na Vesha Okello walikusanyika chini ya chapisho kuonyesha upendo kwake na kumpongeza.

“Ish!” Akothee aliandika.

Rue Baby akasema, “Aaalllllaaaaa eiiii.”

Vesha Okello: Eeeeish yawa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved