•Hivi majuzi wapenzi hao walionekana wakijivinjari pamoja huku Zari akiendelea na ziara yake ya siku kadhaa katika nchi hiyo yake ya kuzaliwa.
•"Nilifanya makosa. Nilikuwa na masikitiko yangu hadi kufikia hatua ya kujitokeza kwenye mitandao ya kijamii. Nilizamia kwenye jukwaa lisilofaa," Zari alisema.
Ndoa ya wapenzi wawili kutoka Uganda, Zari Hassan na Shakib Cham Lutaaya, inaonekana kufufuka tena baada ya wiki kadhaa za wasiwasi.
Hivi majuzi wapenzi hao walionekana wakijivinjari pamoja huku Zari akiendelea na ziara yake ya siku kadhaa katika nchi hiyo yake ya kuzaliwa.
Haya yanajiri baada ya mpenzi huyo wa zamani wa mwimbaji Diamond Platnumz kuchukua hatua ya kuomba msamaha kwa mumewe katika juhudi za kuokoa ndoa yao isisambaratike.
Katika ombi lake la msamaha, Zari alikiri alifanya makosa kwa kupeleka hasira zake kwa mumewe kwenye mitandao ya kijamii wakati wa mzozo wao wiki chache zilizopita.
“Nina mume lakini wakati fulani huko nyuma nilisema mambo ya kushangaza, kama mlivyoona. Kama mtu wa kawaida, unafikia hatua na unapata changamoto. Mambo hutokea, Mwenyezi Mungu alituumba hivyo-sote tunafanya makosa. Lakini ukitafakari unaweza kuona makosa yako,” Zari alisema.
Aliongeza, “Kweli. Nilifanya makosa. Nilikuwa na masikitiko yangu hadi kufikia hatua ya kujitokeza kwenye mitandao ya kijamii. Nilizamia kwenye jukwaa lisilofaa."
Zari alirejea katika nchi yake ya kuzaliwa ya Uganda mwishoni mwa wiki jana kwa safari ya siku kadhaa.
Akizungumza wakati wa mahojiano ya wikendi, sosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 43 alikiri kuwa sababu ya ziara yake hiyo ni kutaka kurudiana na mumewe Shakib ambaye alitofautiana naye hadharani wiki kadhaa zilizopita.
Zari alikiri alifanya makosa kwa kuzungumza vibaya kuhusu mumewe mtandaoni na kulaumu matendo yake kwa masikitiko yaliyomkumba.
"Mambo hutokea. Mungu alituumba ili tufanye makosa. Tunafanya makosa, lakini baadaye unatafakari na kutambua ulivuka mipaka," Zari alisema.
"Mimi ni mwanamke mkaidi. Mimi ni mwanamke anayejitegemea. Mimi ni Zari the BossLady. Lakini, kwa kweli, nilifanya makosa, nilikuwa na madhaiko yangu," aliongeza.
Mama huyo wa watoto watano alikiri kuwa ilifanya makosa makubwa kutumia mitandao ya kijamii kushughulikia masikitiko yake na Shakib.
Aliweka wazi kwamba alifunga safari ya kurudi nchi ya mama yake kimsingi kwa sababu anataka mumewe arudi.
"Niko hapa kurekebisha mambo, nikisema chochote nilichosema kwenye mtandao sio sawa, nakubali, nataka mume wangu Shakib arudi," alisema.
Mwezi uliopita, Zari alizamia kwenye mitandao ya kijamii kumzomea mumewe Shakib na kutishia kumuacha. Hii ilikuwa baada ya Shakib kuonyesha kutilia shaka uhusiano wa Diamond na mkewe.