•Bradley asafiri kwa ndege mara ya kwanza kwenda likizo Diani kwa siku tatu
•Safari yake ya kwenda Mombasa imefadhiliwana na Bonfire Adventures.
Jumanne Septemba 3, Bradley Marongo alipanda ndege mara ya kwanza kwenda likizo Diani.
Hii ni wiki chache baada ya Simon Kabu, mkurugenzi mkuu mtendaji wa Bonfire Adventures kutangaza kuwa atafadhili likizo ya siku tatu ya Bradley kuzuru Mombasa.
Bradley ameweza kupata ubalozi wa mashirika kadhaa ikiwemo ikiwa ni Khushi Motors. Kampuni ya usafiri ya Kabu pia ilijiunga na orodha ya ushirikiano.
Katika video aliyoweka katika mtandao wake wa Youtube, Bradley anaonekana na mkoba wake akiwa katika uwanja wa ndege akielekea kwa ndege.
Anapiga picha na mashabiki wake na baadaye kuenda kupanda gari ambalo lilikuwa likimsubiri.
Akiwa katika uwanja wa ndege, Bradley alisikika akisema "ni mara ya kwanza kuenda kwa ndege....naenda Diani vacation ya siku tatu."
Mashabiki wengi wa Bradley wamefurahishwa na jinsi maisha yake yalivyobadilika huku wengine wakionekana kutofurahishwa na kuuliza ni kwa nini kijana huyo anasafiri kuenda likizo peke yake Mombasa akiwa ameiacha familia yake mashambani.