• Kinuthia afunguka na kusema kuwa ana mpango wa kukuza matiti siku zijazo akipata pesa
• Alikubali kuwa yuko katika uhusiano ambao unakaribia miaka miwili
• Anasisitiza kuwa ni muhimu kuweka maisha yako ya kibinafsi siri
Muundaji maudhui Kelvin Kinuthia amefunguka na kusema kuwa ana mipango ya kukuza matiti siku zijazo.
Kwenye mahojiano na Eve Mungai, Kinuthia alizungumzia kuhusu safari yake ya mapenzi na kueleza kwamba amekuwa katika mahusiano mengi na ya sasa inakaribia miaka miwili.
Alisisitiza umuhimu wa kuweka maisha yako ya kibinafsi siri hata kwa wale wa karibu nawe.
Kinuthia anaamini kuwa kuingiza watu wengine katika uhusiano wako kunaweza leta matatizo na anapendelea kudumisha mipaka.
"Ni mambo yako. Ni wewe ndiye unachumbiana. Utaleta watu kwa uhusiano wako alafu wakuje waharibu"
Alipoulizwa kuhusu kupata watoto, Kinuthia alikiri kwamba hajawai kuwa na mawazo hayo na kusema kuwa kuna uwezekano wake kupata watoto wawili.
"Sijawahi kaa chini nikapiga hesabu ya kuwa na watoto. Inawezekana lakini naona inataka kukaa chini vizuri. Lakini labda wawili wakienda sana"
Kinuthia aliongezea kuwa ana hamu ya kukuza matiti siku zijazo kwani amekuwa akiifikira kutoka mwezi uliopita.
"Mi hata kuna upasuaji nataka kwenda...navaanga nguo zinakosa mahali pa kushikilia...Si kitu kubwa lakini kitu"
Alieleza kuwa amefanya utafiti na bei ilimshtua lakini akipata pesa hizo ataenda kukuza matiti. "Gharama ndio ilinishtua...About one point something million. Hiyo ni deposit ya gari mzima...nikipata pesa mzuri nitaenda"
Kuja kwake wazi kuhusu uhusiano wake umekuja wiki moja baada ya yeye kufafanua kuwa hayuko katika uhusiano wowotwe na rafiki yake mwigizaji Shiphira.