Binti wa Jacob Zuma kuolewa na Mfalme Mswati kama mke wa 16

Binti wa miaka 21 wa Rais wa zamani ,Jacob Zuma, anatarajiwa kuolewa na Mfalme wa Eswatini Mswati III kama mke wake wa 16

Muhtasari

•Nomcebo Zuma alitolewa kama mchumba wa Mswati III wakati wa sherehe iliyopewa jina Umhlanga au densi ya Reed mnamo Jumatatu Sep 2.

•Kulingana na wachapishaji wengi wa Afrika Kusini, binti huyo atatambulishwa kwa mama ya mfalme katika wiki zijazo.

Mfalme Mswati III
Image: HISANI

Binti wa miaka 21 wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma anatarajiwa kuolewa na Mfalme wa Eswatini Mswati III kama mke wake wa 16.

Nomcebo Zuma alitolewa kama mchumba wa Mswati III wakati wa sherehe iliyopewa jina Umhlanga au densi ya Reed mnamo Jumatatu Sep 2.

Mfalme Mswati ana miaka 56.

 Umhlanga au Reed Dance iliundwa katika miaka ya 1940 na Mfalme Sobhuza II kwa ajili ya Mfalme kuchagua mke mpya kila mwaka.

Wakati wa sherehe, wasichana wachanga husherehekea ubikira wao katika Kijiji cha Kifalme cha Ludzidzini huko Lobomba, Ufalme wa Eswatini.

Kulingana na wachapishaji wengi wa Afrika Kusini, binti huyo atatambulishwa kwa mama ya mfalme katika wiki zijazo.

Wawakilishi wa Wafalme mnamo Julai walitembelea nyumba ya Zuma katika eneo la Nkandla kuwasilisha ng'ombe kama sehemu ya mahari.

Pendekezo hilo lilirasimishwa kupitia sherehe ya kitamaduni inayojulikana kama "kucela," ambapo Mfalme hutuma timu kuwasilisha zawadi kuashiria ombi lake au ruhusa ya kuoa msichana husika.

Mazungumzo yanabaki kuwa siri hadi sasa.