Salasya ataka ushauri wa kuboresha mchezo wa kitandani kabla ya kukutana na Huddah Monroe

Aliomba ushauri kuhusu aina ya chakula anachohitaji kula ili kuhakikisha kwamba mchezo wake wa kitandani ni wa hali ya juu

Muhtasari

•Alionyesha machapisho ya Huddah Monroe kwenye ukurasa wake na kujigamba kuhusu mambo ambayo mrembo huyo alikuwa ameandika kwenye Instastori zake.

•Mbunge huyo wa muhula wa kwanza aliendelea kueleza kuwa kwa kweli ndoto yake siku moja inaweza kutimia.

HUDDAH NA SALASYA
HUDDAH NA SALASYA
Image: HISANI

Siku ya Jumamosi, mwanasiasa mwenye utata Peter Kalerwa Salasya alijibu kwa msisimko baada ya crush wake Huddah Monroe kuandika baadhi ya machapisho kwenye Instagram yaliyodokeza kuhusu kupendezwa kwake naye.

Mbunge huyo wa Mumias Mashariki ambaye amekuwa akieleza waziwazi mapenzi na kuvutiwa kwake na sosholaiti huyo mrembo hakuweza kuficha furaha yake baada ya kugundua jinsi ndoto yake ya muda mrefu inavyokaribia kuwa ukweli.

Alionyesha machapisho ya Huddah Monroe kwenye ukurasa wake na kujigamba kuhusu mambo ambayo mrembo huyo alikuwa ameandika kwenye Instastori zake.

“Anahitaji uponyaji wa mapenzi!! Anahitaji mtu wa kumpenda!!! Hawezi kushikilia kwa muda mrefu zaidi !!! machapisho ya kupendeza sana hapa kwangu," Salasya aliandika chini ya screenshot za machapisho ya Huddah.

Mbunge huyo wa muhula wa kwanza aliendelea kueleza kuwa kwa kweli ndoto yake siku moja inaweza kutimia.

Pia aliomba ushauri kuhusu aina ya chakula anachohitaji kula ili kuhakikisha kwamba mchezo wake wa kitandani ni wa hali ya juu kabla ya kukutana na  crush wake.

“Hii kitu inaeza kuwa ukweli siku moja mimi mwenyewe nikimpata Msichana huyu kwa kweli,” Salasya aliandika.

Katika machapisho yake, sosholaiti Huddah Monroe alikuwa amedokeza kuhusu kukubali mapenzi ambayo Salasya amekuwa akimuonyesha.

Pia alidokeza kuwa tayari kulala na mwanasiasa huyo kijana.

"Nataka uponyaji wa kimapenzi, nahitaji kupendwa, na mpenzi siwezi kuvumilia kwa muda mrefu," Huddah aliandika.

Aliambatanisha machapisho yake na picha za Salasya.