Nicki Big akiri haamini katika mapenzi

Nicki pia alipasua mbarika kuwa kamwe hatawai oa.

Muhtasari

• Mchekeshaji Nick BigFish amesema kuwa kamwe haamini katika mapenzi akieleza kuwa ni utapeli.

Image: INSTAGRAM// NICKY BIGFISH

Mchekeshaji Nick BigFish amesema kuwa kamwe haamini katika mapenzi akieleza kuwa ni utapeli.

Big Fish ambaye hufanya video za mzaha mtandaoni amekiri kuwa kulingana na utafiti alioufanya mwenyewe amegundua kuwa ndoa ambazo zimedumu ni za wahusika ambao walijipanga na mwanzoni walikuwa tu marafiki wa kawaida.

"Mimi nimekuwa nikiweka mambo yangu wazi kuwa siamini katika mapenzi, asilimia mia. Mapenzi ni utapeli lakini wale waliokomaa katika mapenzi sisemi ati ni kitu kibaya lakini nawatakia mema lakini kwangu mimi siamini katika mapenzi." Alisema BigFish.

BigFish aidha hakuweka wazi msichana aliyemuumiza roho na kumfanya kuogopa kuwa katika mapenzi.

Nicki pia alipasua mbarika kuwa kamwe hatawai oa.

Hata hivyo, mchekeshaji BigFish amesifia ndoa za wazazi kuwa zimekuwa kwa muda mrefu kwa sababu ndoa zao zilipangwa mapema.

"Nimekuja kuona kama ndoa za wazazi wetu, nyingi zao zilikuwa zimepangwa  na mwanzo hakukuwa na mapenzi na ndio sababu zimekuwepo kwa muda mrefu." Alisema BigFish.

Wakati huo pia, Nicki BigFish amekiri kuwa mwaka wa 2024 ndio umekuwa mbaya zaidi katika miaka yote aliyoishi duniani.

Amekiri kuwa baba wake mzazi, mtoto wake na nyanya yake waliaga dunia matukio ambayo yalimuathiri sana kisaikolojia.