Mahakama moja nchini Ugiriki, imemhukumu kifungo cha mwezi
mmoja jela jamaa mmoja aliyedaiwa kuwakosesha jirani zake amani kwa kupenyeza
mara kwa mara kwa boma lao na kunusa viatu.
Akiwa mbele ya korti ya Thessaloniki, jamaa huyo mwenye umri
wa miaka 28 alishindwa kujitetea kwa kueleza tabia yake ya kunusa viatu vya jirani
zake japokuwa alisema tabia hiyo imemtia aibu kubwa sana.
Mshukiwa huyo alikiri kuwa hakuwa na nia ya kuvunja sheria
wala kumdhuru mtu yeyote katika kutekeleza kosa hilo la kuwakera jirani zake na
kwamba hakufahamu ni kwa nini alikuwa anatekeleza kisa hicho.
Hata hivyo walalamishi waliiambia korti kuwa jamma huyo hakuonyesha
ishara yoyote ya uchokozi wakati wa ziara zake za usiku katika boma lao.
Mshukiwa huyo alikamatwa na polisi akiwa mbele ya nyumba ya mlalamishi akinusa viatu vilivyokuwa
vimewachwa nje usiku mmoja baada ya mlalamishi kujulisha polisi kuhusu kisa
hicho.
Mahakama ya Thessaloniki iliambiwa kuwa kulikuwepo visa zaidi
ya mara tatu vya jamma huyo kukosesha jirani zake amani katika muda wa miezi
sita iliyopita licha yawalalamishi kutoa taarifa kwa familia ya mshukiwa kutaka
kumkomesha.
Tatizo hilo lilikadiriwa kumalizikia mahakamani baada ya walalamishi
kukosa kupata suluhu kufuatia malalamishi yao kwa familia ya mshukiwa.
Hata hivyo, mshukiwa atatakiwa kuhudhuria vikao
vya matibabu ilikupata ushauri nasaha wa kurekebisha tabia hiyo iliyomweka mashakani.