Mchekeshaji YY amesema kwamba mwanamume hafai kukaa zaidi ya miezi sita bila mpenzi baada ya kuachana.
YY alisema hayo katika mahojiano na kituo kimoja cha burudani cha humu nchini alipoulizwa sababu iliyomfanya kuingia katika uhusiano mwingine na Noela chini ya mwezi mmoja baada ya kuachana na mama wa mtoto, Marya Okoth.
“Kitu kimoja ninachofahamu ni kwamba mwanamume ukijipatia mapumziko hata ya miezi 6 kutoka kwa mahusiano ya muda mrefu, hautawahi piga hatua ya mbele na hautawahi taka mambo ya wanawake.” Alisema YY.
Tangu kuwachana na Marya, YY amekuwa akichapisha video na picha kwenye akaunti zake za mitandao akiwa na mpenzi wake mpya.
YY aliendelea kusema kuwa mwanaume anayechukua muda mrefu wa mapumziko baada ya kuwachana na mpenzi wake huwa na ugumu kurejea tena katika mapenzi.
“Ukijaribu kukaa kwa zaidi ya miezi sita bila ya kuwa katika mahusiano, hutataka tena mchumba katika maisha,” aliongeza.
Jumanne wiki iliyopita mchekeshaji huyo aliwatembelea wazazi wa mpenzi wake mpya nyumbani kwao katika kijiji cha Kamukuywa kaunti ya Bungoma.
YY alichapisha video kwenye mtandao wake wa Instagram na maandishi kuwa ‘asante kunitembeza katika nyumba ya babako’ akiashiria shukrani kwa mpenzi wake mpya katika video waliokuwa wakitembea kutoka nje ya nyumba.
“Mwanamume kamili lazima akutane na wazazi ili kuwasilisha nia yake,” aliandika YY kwenye matukio yake ya Instagram(stories).
YY amekuwa akichapisha mtandaoni picha na video akiwa na mpenzi wake baada ya kuwachana na Marya.
Mchekeshaji huyo aliweka wazi kukatika kwa mahusiano na mama wa mtoto wake akisema kuwa ijapokuwa walikuwa wameona, ni vyeti vya kuhalalisha ndoa vilikuwa havipo.