logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Natalie Githinji azungumzia hofu ya kufa kutokana na Endometriosis

Alikiri kuwa aliathiriwa na kifo cha Jahmby Koikai ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu aliyeaga dunia akipambana na ugonjwa wa endometriosis.

image
na Achieng' Kezia

Dakia-udaku29 October 2024 - 08:55

Muhtasari



    • Natalie aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa endometriosis mnamo 2016.

Mtangazaji wa zamani wa NRG Radio, Natalie Githinji afunguka na kusema kuwa ana hofu ya kufa kutokana na ugonjwa wa endometriosis ambao anauguza.


Kwa mahojiano na watangazaji wa Homeboyz Radio, Lotan na Tonio, Natalie alifunguka na kuelezea hofu yake.


“Huwa unaogopa?” Lotan aliuliza.


“Kwamba nitakufa, ndio…Bado naogopa, nahisi kama naeza kuishia nimeaga na ndio maana naishi maisha yangu kikamilifu kila siku nyingine ninapopata nafasi. Kwa sababu kama hakuna tiba, hiyo inamaanisha hatimaye...” Natalie alijibu.


Alikiri kuwa aliathiriwa na kifo cha Jahmby Koikai ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu aliyeaga dunia akipambana na ugonjwa wa endometriosis.


“Niliogopa na nilikuwa kazini. Ninahisi kwamba hapo ndipo nitakaposihia, jambo ambalo linatishia,”


Natalie anashauri wanaume ambao wanachumbiana na wanawake walio na endometriosis kuwa na subira kwao kwani huwa hawapati usaidizi ambao wanahitaji na kuwaambia wanawake ambao wana endometriosis kuishi maisha na kupigana kila siku na kuwa siku moja huenda wakapona.


“Ikiwa unachumbiana na mtu aliye na endometriosis, uwe na subira kwake. Hatimaye, anaweza kupona. Hatupati usaidizi tunaohitaji kila wakati. Mimi hupata usaidizi mkubwa zaidi kutoka kwa mama yangu na marafiki zangu. Ikiwa wewe ni mwanamke unapitia endo, pigana kila siku na uishi maisha," aliongeza.


Natalie aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa endometriosis mnamo 2016.


Anatamani angejua kuhusu hali hiyo mapema, kwani alivumilia maumivu makali kabla ya kufanyiwa utambuzi.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved