logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize aomba kukutana na mzee aliyekiri kufilisika kwa kupenda warembo wenye ‘mizigo’

Harmonize naye ni kama Mzee Makosa ambaye anapenda sana wanawake ambao wamebarikiwa na viuno vipana.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Dakia-udaku31 October 2024 - 11:07

Muhtasari


  • Mzee Makosa alivuma baada ya kufanya mahojiano akikiri kwamba alipoteza utajiri wake wote na sasa ni maskini asiye na mbele wala nyuma.
  • Mzee huyo baada yakupokezwa zawadi ya pesa na Diamond, alifanya mahojiano ambapo alizungumzia jinsi utajiri wake ulivyoyeyuka.

Siku moja baada ya Diamond Platnumz kukutana na Mzee Makosa na kumzawadi kitita cha shilingi milioni 10 za kitanzania, Harmonize naye ameomba kukutana na mzee huyo.

Mzee Makosa alivuma baada ya kufanya mahojiano akikiri kwamba alipoteza utajiri wake wote na sasa ni maskini asiye na mbele wala nyuma.

Mzee huyo baada yakupokezwa zawadi ya pesa na Diamond, alifanya mahojiano ambapo alizungumzia jinsi utajiri wake ulivyoyeyuka.

Alikiri kwamba enzi za utajiri wake, alikuwa anapenda sana warembo wenye viuno vipana na baada ya pesa kuisha, wote walichimba mitini na kumuacha kwenye mataa mzee wa watu.

Akimtambulisha mke wake, Mzee Makosa alisema, “Huyu ndiye mke wangu ambaye ndiye anayelea kabisa maisha ya Makosa.Tunayo miaka 30 pamoja, kama ni kuchukizana tumechukizana sana na kama ni kupatana tumepatana sana.”

“Kwa hivyo kama ni kubaki kabaki yeye tu. Walikuwepo wenye mizigo, lakini hela zilipokauka, kila mtu aliondoka na mzigo wake,’ aliongeza.

Ni kutokana na kukiri huku ambapo Harmonize alivutiwa na kutaka kukutana naye ili kupata kujifunza kitu.

Harmonize naye ni kama Mzee Makosa ambaye anapenda sana wanawake ambao wamebarikiwa na viuno vipana.

“Naomba kuonana na huyu mzee tafadhali, hapo kwenye walikuwepo wenye mizigo pamenishtua. Nina la kujifunza. Halafu ni kweli huwa wanaondoka na mizigo yao,’ Harmonize alisema.

Mzee Makosa jinsi anavyofahamika na watu wengi, katika mahojiano na kituo kimoja nchini Tanzania alieleza jinsi aliingia kwenye dimbwi la umaskini kutoka kwenye utajiri aliokuwa nao.

Platnumz aliguswa na simulizi ya mzee huyo na alitaka sana kukutana naye kwa mazungumzo na angalau apate fursa ya kumsalamia mkononi.

Aidha baada ya kupata fursa ya kukutana na Mzee Makosa na hata kuwa na nafasi ya kuzungumza naye jinsi alivyokuwa ametamani, Diamond Platnumz hatimaye alikabidhi kitita cha shilingi milioni 10 mzee huyo.

Baada ya kupokezwa hela hizo Mzee Makosa alisema kuwa msanii huyo alimfanyia kitu ambacho hakijawai kufanywa kwa ajili yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved