Mwanashoshalaiti Huddah Monroe amewashauri Wakenya
wanaoagiza samani kutoka nchu za ughaibuni kuwacha kununua makochi kutoka nchi
za nje na badala yake kununua samani kutoka kwa wafanyabiashara na fundi
wanaotengeza bidhaa hiyo humu nchini.
Huddah amesema kuwa kitu kibaya sana unaweza kuagiza kutoka
nchi za ughaibuni ni samani akiashiria kuwa unaweza dhani ni bei nafuu kumbe
sivyo.
Kwa mujibu wa Huddah, samani inaweza kuchukua shehena moja
ya usafirishaji wa mizigo kuingia ndani ya nchi ambayo inagharimu kati ya
shilingi elsfu sitini na elfu sitini na tano.
Mwanashoshalaiti huyo amejutia namna aligharamika kuagiza
samani kutoka nchi ya nje badala ya kumpiga sapoti rafiki wake aliyekuwa na bidhaa
sawia na ile aliyokuwa ameagiza. Huddah amesema kuwa alinunua sofa moja kutoka
Dubai kwa Dirham 1000 sawia na shilingi takribani 35,000 za Kenya akidhania ni
bei nafuu.
Wakati wa kuisafirisha Kenya, Huddah amesema kuwa alijutia
kiwango cha fedha alizolipa kwani kochi hiyo ilichukua nafasi yote ya mita za
ujazo yaani cubic meter na kulipia shilingi elfu sitini na tano.
Mwanashoshalaiti huyo aidha amewataka Wakenya kuwacha kuagiza
samani kutoka ughaibuni.
“Ujinga kamili. Nunua samani kutoka kwa watu wa nyumbani. Sofa huuzwa
ata shilingi 55,000.” Aliandika Huddah Monroe kwa ukurasa wake wa
Instagram.
Vile vile, Huddah alisisitiza kuwa ikiwa si kitu cha kipekee
ambacho hakipatikani Kenya, aliwataka Wakenya kuwacha kununua samani kutoka
nchi za nje.