Mchungaji maarufu James Maina Ng’ang’a anawataka watu walio na
nywele mtindo wa rasta kwanza kuzinyoa ili waweze kufika katika kanisa lake.
Katika video ya hivi majuzi aliyochapishwa kwenye TikTok,
Ng’ang’a alisema kwamba wale ambao wana nywele mtindo wa rasta wanyoe na ikiwa
yeyote ambaye ana rasta atamkaribia atamnyoa la sivyo hatoingia kwa kanisa lake
na ikiwa ataingia itakuwa Jumapili moja pekee.
“We kama uko na rasta nyoa, utanyoa. Ukija mahali niko
nitakuonyoa kama si hivyo hutaingia, utaingia Sunday moja hiyo ingine
nitakunyoa,” alisema.
Mchungaji huyo pia alisisitiza kwamba ni wanawake ndio
wameharibu kanisa lake kwani wanakuja na mavazi ambayo sio sawa kuvaliwa
kanisani.
“Wamama nyinyi ndio mmeharibu kanisa hii na mnaweka rangi ni
sawa, na kipaza sauti na huko umevaa suruali ile imevaliwa na koinange what is
that eh? Huko unafanya vitu ambavyo ni vya kule nje lakini mdomo tu ndio Bwana
asifiwe! Basi wewe ni muuwaji, we ni mwongo, we ni msengenyaji, we ni mwizi, we
huna akili ya Mungu, akili zako ziko dunia, huna upendo, huna ushirika na roho
wa Mungu, unaongea tu kila saa mambo ya serikali,”
Anawashauri wahubiri kufunza kuhusu ufalme wa mbinguni na sio
pesa kwani pesa wataziacha humu duniani.
“Kuna Mungu juu mbinguni. Wale wameokoka, wale upcoming
preachers preach about the kingdom of God not about the money. Pesa ni takataka
tu utaziwacha tu. Dunia itakuhangaisha ikuhangaishe hutalala, ukipata milioni
mbili unataka tano,”