logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwijaku awataka wasanii wa Tanzania kukubali ‘challenge’ kutoka kwa Kaligraph Jones

Kaligraph Jones alizua gumzo mtandaoni kutokana na nyumba yake aliyoichapisha mtandaoni

image
na Brandon Asiema

Dakia-udaku15 November 2024 - 11:23

Muhtasari


  • Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wametoa mseto wa hisia kutokana na nyumba wa msanii huyo kuwa kubwa.
  • Mwemba Burton maarufu kama Mwijaku amewataka Wakenya kuheshimu nyumba ya Jones akiahidi kumtembelea siku za hivi karibuni.

Mtangazaji na mshawishi wa mitandaoni kutoka Tanzania

Mwanahabari wa Tanzania Mwemba Burton maafufu kama Mwijaku amekubali challenge kutoka Kenya ya wasanii kuchapisha nyumba zao kwenye mtandao wa kijamii.


Mwijaku amesema hayo baada ya msanii kutoka Kenya Kaligraph Jones maarufu kama OG kuchapisha picha za nyumba yake mpya mtandaoni jambo ambalo lilizua gumzo katika mitandao ya kijamii nchini Kenya.


“Challenge accepted! Wasani wa kitanzania, Kaligraph kutoka Kenya jamani unajijua mwenyewe mdogo wangu naona lile ni hekalu, wasanii wa Tanzania naomba tumjibu Kaligraph.”  Alisema Mwijaku.


Hata hivyo Mwijaku amewapa wasanii wa Tanzania changamoto ya kuingia katika challenge ya kuchapisha picha za nyumba zao mtandaoni.


Mwijaku amesifia nyumba aliyojenga Kaligraph Jones akilifananisha na kasri la mabilioni ya pesa akiwa amepiga magoti akisema ‘igweee igweee igweeee igweee’ huku akikubali kunyoroshwa na msanii huyo wa Kenya katika kumiliki nyumba.


Katika video aliyochapisha kwenye mtandao wake wa kijamii, Mwijaku ameahidi kumtembelea Kaligraph Jones.


Aidha, mwanahabari huyo kutoka Tanzania ambaye pia ni mshawishi wa mitandaoni amewataka Wakenya kuheshimu jumba alilojenga OG.

Mitandao ya kijamii nchini ilijaa jumbe za kutania nyumba ya Jones kutokana na ukubwa wa nyumba hiyo huku OG akifutilia mbali kauli za Wakenya akisema kuwa huo ndio ukosoaji alikuwa anaomba Mungu ambariki nao kutoka kwa watu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved