Msanii Octopizzo ametofautiana na seneta wa Nairobi Edwin
Sifuna baada ya seneta huyo kutetea
makasisi wa kanisa Katoliki katika kuwajibisha serikali ya rais William Ruto.
Seneta wa kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna kwenye mtandao wa X
ametetea muungano wa makasisi wa kanisa Katoliki waliotoa taarifa ya kukashifu
utendakazi wa serikali.
Katika kumjibu seneta Sifuna, msanii Octopizzo ametofautiana
na seneta huyo akisema kuwa kanisa Katoliki halikuzungumza wakati baadhi ya vijana
wa kizazi cha Genz Z waliuliwa katika maandamano ya kupinga mswada wa fedha wa
2024 mwezi wa Juni.
Kwa mujibu wa Octopizzo, amewalaumu makasisi kwa kukosa
uthabiti wa kuwajibisha serikali mara kwa mara akisema kuwa makasisi hao wanahisi
kutengwa na sasa wana shauku ya kudai sehemu ya faida ambazo maaskofu wengine
wanapokea.
Octopizzo ameongeza kusema kuwa watu wanatoroka makanisani kwa
kuwa wanahisi kanisa limegeukia biashara kutoka kwa pahala patakatifu pa
kiroho.
Kwa upande wake seneta Sifuna, Kanisa Katoliki limekuwa
mstari wa mbele katika kukosoa utendakazi wa serikali likitoa taarifa ya mara kwa
mara kuhusu vilio vya Wakenya katika mambo ambayo serikali inatekeleza
inayoonekana kuwakandamiza.
Seneta Sifuna amesema kuwa ijapokuwa yeye si Mkristo mzuri Zaidi,
wakati mwingine shetani humkalia mara kwa mara lakini licha ya hiyo anajivunia
kuwa mshiriki wa kanisa Katoliki ambalo limekuwa imara kupinga matukio ambayo
si ya haki nchini. Sifuna amesema kuwa makasisi wa kanisa Katoliki huwa wanazungumza
mambo yanayomhusu hivyo basi naye pia atazungumza kwa ajili yao.
“Mimi si Mkristo mzuri, shetani hukanilia mara kwa mara lakini
ninajivunia kanisa langu kwa sababu limekuwa thabiti kweny misimamo ya kweli.
Maaskofu wanazungumza kwa ajili yangu. Nitazungumza kwa ajili yao.”
Alisema Sifuna kwenye ukurasa wake wa X.
Hata hivyo, Octopizzo amekosoa seneta Sifuna kuwa mnamo
tarehe 25 Juni wakati wa maandamano hawakuhitaji siku 4 kutoa taarifa wakati Zaidi
ya watu 60 wailuawa.
“@edwinsifuna mnamo Juni 25 ilikuwa siku ambayo hawakustahili(makasisi)
siku nne kutoa taarifa wakati watu zaidi ya 60 waliuliwa. Usitubebe ndogo.”
Octopizzo alimjibu seneta Sifuna.